26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MSD YAZINDUA KIFURUSHI CHA UZAZI

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) imezindua kifurushi cha uzazi (delivery pack) kwa ajili ya kuwezesha wajawazito kupata vifaa muhimu vya kujifungulia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 7, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema kifurushi hicho kitapatikana kwa bei ya Sh 21,000.

“Vifaa vyote muhimu tumevikusanya na kuviweka pamoja, humu ndani kuna pamba kubwa, mpira wa kuzuia uchafu, taulo ya kike ya wazazi, sindano ya kuzuia damu kupotea, mipira ya mikono (surgery gloves), nyembe za kupasulia, kibana kitovu cha mtoto, dawa ya spirit, detol ya maji, dawa ya sindano ya ganzi, mabomba ya sindano na nyuzi za kushonea,” amesema.

Amesema kati ya vifaa vyote hivyo, mpira wa kuzuia uchafu ndio ambao huuzwa gharama zaidi ya Sh 13,700 na kwamba mfuko unaohifadhi vifaa hivyo hauingizi maji na unadumu hadi miaka mitano.

Pamoja na mambo mengine, amesema seti hii ya vifaa mtaani inauzwa kati ya Sh 55,000 hadi Sh 60,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles