28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

Msako wanaotumia ombaomba kupata fedha wadaka 56

Tunu Nassor na Christina Gauluhanga -Dar es salaam

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam imewakamata watu 56 wanaotumia shughuli ya ombaomba kama chanzo cha mapato yako.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake jana, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo, Joyce Maketa, alisema kati yao 30 ni wakubwa na watoto ni 26.

Joyce alisema kati yao, watoto 12 walipelekwa makao  yaliyopo Msongola na mmoja ambaye ni mlemavu mwenye umri wa miaka 11 alisamehewa.

Alisema watoto wawili wazazi wao walilipa faini ya Sh 50,000 kila mmoja na wengine 12 walipelekwa Vingunguti.

“Oparesheni ya kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria ombaomba bado inaendelea ambapo Ijumaa tumefanikiwa kuwakamata watu hawa na watachukuliwa sheria inayostahili ili kupunguza vitendo hivi, ikiwamo uchafuzi wa mazingira,” alisema Joyce.

Alisema kwa upande wa watu wazima, tisa walifikishwa jana katika Mahakama ya Jiji ambapo wameshtakiwa kwa makosa ya uchafuzi wa mazingira kinyume na sheria.

“Hawa tisa tumewafikisha mahakamani kwa kuwa wametoka mkoani Dodoma kwa lengo la kuja kuomba hapa Dar es Salaam,” alisema Joyce.

Alisema nane ambao walikuwa wazee kupita kiasi na wengine nane waliokuwa na matatizo ya kiafya walisamehewa.

“Watano waliokuja kuomba katika nyumba za ibada tuliwaelimisha na kuwapa onyo kali, hivyo hatutarajii kama watarudia kosa hilo,” alisema Joyce.

Hata hivyo, alisema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za kuomba kwani wengi, hasa ambao walienda kwenye nyumba za ibada kuomba wanaamini ni haki yao kimsingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles