28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

DPP azipa kazi kamati Jukwaa la Jinai

Mwandishi Wetu- Tabora

MKURUGENZI wa Mashtaka Tanzania (DPP), Biswalo Mganga, amezitaka kamati za Jukwaa la Jinai kuanzia wilaya hadi mkoa kuhakikisha wanaweka mikakati ya kupambana na vitendo vya uhalifu wakati wote na kipindi cha kampeni na uchaguzi ili wananchi waendelee kuishi kwa amani.

Alisema kamati ni vema wakaandaa mikakati ya kukabiliana na matatizo madogo madogo mapema, badala ya kusubiri Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ndiyo hatua zichukuliwe.

Biswalo alitoa kauli hiyo jana, wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo mkoani hapa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa kesi za rushwa na udanganyifu.

Alisema ni vema jukwaa hilo likasaidia jamii itambue umuhimu wa kuishi kwa amani na kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Biswalo alisema kuna watu wana dhana potofu ya kusema Serikali haina fedha, inawatoza wahalifu ili ipate fedha za kuendesha shughuli zake.

Alisema dhana hiyo ni potofu kwani hata nchi zilizoendelea zimekuwa na utaratibu wa kuwatoza adhabu kwa wahalifu wanaokiri makosa yao.

Biswalo alisema hata vitabu vitakatifu vimeandika kuwa mtu anayekutwa na kosa anapaswa alipe mara mbili ya alichochukua.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alisema Serikali itahakikisha inaweka mazingira wezeshi kuhakikisha jukwaa hilo linasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu kama vile mauaji ya wazee na uhalifu mwingine.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles