27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MRADI WA MAJI MAFIA WAZINDULIWA

 

                                                                  |Tunu Nassor, Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amezindua mradi wa ufungaji wa pampu mpya katika chanzo cha maji cha Kilindoni Wilayani Mafia mkoani Pwai.

Mradi huo umetekelezwa na Malaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) kwa gharama ya Sh milioni 52.7 ikiwa ni utekelezaji wa agizo lake alipoiomba mamlaka hiyo kusaidia kazi hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Aweso ameipongeza Dawasa kwa kutekeleza agizo alilolitoa kwa muda mfupi ambapo kazi hiyo imekamilika.

“Pamoja na kuongeza uzalishaji wa maji pampu hizi mpya zimepunguza matumizi ya umeme mara dufu na hivyo kuipunguzia gharama za uendeshaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Maingira Kilindoni (Kiuwassa).

“Naipongeza Dawasa kwa kazi nzuri na nitasimama popote kuwaelezea kuwa mnaweza katika utendaji kazi. Nitasimama  katika vikao vyetu na kuwasemea kuwa mnaweza na mnatosha kwani ukizaa mtoto anafanya vizuri kazi yako ni kumwombea dua,” amesema Aweso.

Aidha, Aweso amesema pamoja na kuwafungia pampu Kiuwasa anaomba Dawasa kuwapelekea mita za maji ili waweze kukusanya mapato.

“Wananchi wamekuwa wakikadiriwa Ankara zao za maji hivyo Dawasa niwaombe tena kuwanunulia mita ili kuondoa malalamiko ya kubambikiziwa Ankara,” amesema Aweso.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles