*Ni wimbo wakwanza wa Choplife Soundsystem
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Baada ya kutangaza habari kubwa za ujio wa project ya Afrodance Soundsystem, wasanii wakubwa wa muziki, Mr Eazi na DJ Edu wameachia ngoma ya kwanza kwenye project hiyo iitwayo Wena ambao pia umemshirikisha mwanamuziki wa Afrika Kusini, Ami Faku.
Mr Eazi amenukuliwa akisema: “Narudi kule nilipoanza, nitafanya tamasha kubwa kwenye vyuo vikuu, uko ndiko nilipoanzia kuimba. Natarajia kwa furaha kubwa kuanza safari hii mpya, na nina shauku kubwa ya kuona muziki mzuri ukianza kutoka na kusindikizwa na uzoefu wake wa moja kwa moja,” amesema.
Wimbo huu uliotolewa na Choplife Limited Aprili 28, unaonyesha jinsi Afrodance mpya ilivyosukwa na DJ Tárico ambayo ni mwendelezo wa kazi za Amapiano za Eazi katika nyimbo zake za hivi karibuni.
Ndani yake ameshirikishwa Ami Faku, mmoja kati ya wasanii wanaosikilizwa zaidi nchini Afrika Kusini, ambaye anatoa ujumbe wenye kugusa moyo kwa lugha ya Xhosa, huku Eazi akijibu kwa Kiingereza.
Ujumbe uliomo ni hadithi ya wapenzi wanaotaka kuwa pamoja lakini hawajapata kufikia malengo yao, ambayo ni janga ambalo linaweza kutatuliwa tu kwa kuchezwa jukwaani.
Wena utaachiwa rasmi Mei 28, ikiwa katika mkusanyiko uliopewa jina la ‘Choplife Vol. 1: Mzansi Chronicles’ ambapo wameshirikishwa wazalishaji muziki maarufu na ma-DJ wa kiwango cha juu.