27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wameshauriwa kujiunga kwenye vikundi ili wapate mitaji

Na Clara Matimo, Mtanzania Digital

Wakulima wameshauriwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali  ikiwemo mikopo inayotolewa na serikali pamaoja na wadau wa kilimo.

Ushauri huo umetolewa na wadau wa kilimo kwa nyakati tofauti walipokuwa wakizungumza na wakulima pamoja na viongozi ngazi ya halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwenye kongamano la uendelezaji sekta ya kilimo pamoja na jinsi ya wakulima kunufaika kwa fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Baadhi ya washiriki wa kongamano la uendelezaji sekta ya kilimo pamoja na jinsi ya wakulima kunufaika kwa fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Kongamano hilo liliandaliwa kupitia mradi wa Tufuatilie kwa Pamoja Rasilimali za Umma’, unaotekelezwa  na Shirika lisilo la kiserikali  linalojishughulisha na Uchumi wa Nyumbani (TAHEA) kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS) katika Kata za Iligamba, Kazunzu na Nyakalili.

Mwezeshaji katika kongamano hilo  Athanas Evaristi aliwaambia wakulima kwamba wakijiunga kwa pamoja itawawezesha kupata kwa urahisi huduma ya elimu kutoka kwa maafisa ugani, kutafuta soko la pamoja na kupata mitaji ya kuendeleza kililo chao.

“Tumeona changamoto ya elimu ya kanuni za kilimo bora kwenye kata kuna afisa ugani mmoja wakati wakulima wako zaidi ya 360  kata ina watu zaidi ya 1,000 hadi 2,000 hivyo afisa ugani hawezi kumtembelea mkulima mmoja mmoja hata kama ni kwa mwaka mzima akawafikia wote lakini wakiungana watapewa elimu kwa pamoja kupitia umoja wao.

“Pia wakiungana wanakuwa na sauti moja wanaweza kupata fursa na utaalamu kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata pembejeo na mitaji inayowezeshwa kwa pamoja huo ni ushauri wangu, unganisheni nguvu ili mpate huduma hizo hata serikali ya awamu ya sita inautashi sana wa kuwahudumia wakulima lakini mkiwa kwenye vikundi maana mkiwa  mmoja mmoja haitawafikia kwa urahisi.

“Meneja Mradi wa ‘Tufuatilie kwa Pamoja Rasilimali za Umma’ kutoka TAHEA, Bundala Ramadhani alisema”Ili mlime kwa tija lazima muwe na mfumo rasmi unaowaunganisha umoja wenu utawawezesha kupata mikopo ambayo itawanufaisha maana mtaweza kununua vitendea kazi ikiwemo  mashine za kusindika mazao ili kuongeza thamani kwenye mazao mnayolima,” alishauri Evaristi.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Buchosa, Grace Machunda aliwahamasisha wakulima kujiunga kwenye vikundi ili wawe na nguvu kubwa ya kuaminika na kukopesheka.

“Naendelea kuwahamasisha wakulima mjiunge katika vikundi kuanzia watu watano na kuendelea mkijiunga mtapata fursa ya mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri pia serikali imetoa fursa ya mikopo kutoka wizarani ya mwanamke mmoja mmoja pamoja na wanawake waliojiunga kwenye vikundi kuanzia watu watano na kuendelea.

“Kwa hiyo wakulima mnaweza kuwasiliana na ofisi ya maendeleo ya jamii tutawaelekeza jinsi ya kuomba mkopo uwe wa mtu mmoja mmoja au wa vikundi kutoka wizarani fursa hizo zipo kinachotakiwa ni mjiunge kwenye vikundi ili muwe na nguvu ya umoja mfanye uzalishaji mzuri wenye tija,”alisema Grace na kuongeza:

“Mkifanya uzalishaji wenye tija wataalamu wa maendeleo kutoka halmashauri wakija kuwatembelea wakaona mnafanya uzalishaji wenye tija itawasaidia kwa kuwapa mikopo kutoka kwenye hiyo mifuko,”alisema Grace.

Hata hivyo wakieleza sababu zinazofanya kilimo chao kisiwe na tija baadhi ya wakulima akiwemo, Costansia Faida na Boniphace Maseswa wa Kata ya Kazunzu na Valeria Ngotezi Kata ya Nyakaliro wamesema ukosefu wa mitaji ndiyo unaosababisha washindwe kufikia malengo yao kwa kulima kilimo chenye tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles