Na Ashura Kazinja, Morogoro
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Tazani Mndeme (35) mpiga debe wa kampuni ya mabasi ya BM Coach kituo cha Msamvu mkoani Morogoro, amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu kifuani na Abdilah Yassin (32) mpiga debe wa mabasi ya kampuni ya Abood wakigombea abiria.
Akizungumza leo Machi 28, na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro FortunatusMusilimu amesema tukio hilo limetokea Machi 28 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika stendi kuu ya mabasi Msamvu Manispaa ya Morogoro baada ya kuzuka ugomvi wa kugombea abiria Kati yao.
Kamanda Musilimu amesema Tazani alichomwa kisu kifuani upande wa kushoto hali iliyopekekea kukimbizwa katika hosoitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha iuhifadhia maiti cha hosoitali ya Rufaa Morogoro na kwamba mtuhumiwa Abdilah maarufu kama Hajamonga Bonge mkazi wa Kihonda amekamatwa na hatua za kumfikisha mahakamani zitafuata upelelezi utakapokamilika.
Hata hivyo Musilimu amewataka mawakala mawakala wa mabasi na wapiga debe wa mabasi (Nasarange) kutokugombea abiria wanaoingia stendi, badala take wawaelekeze katika mabasi ya makampuni yao, napia kuacha kuingia na vitu hatarishi kama visu, bisibisi, nyembe na sime.
Aidha amewataka kuvaa sare na vitambulisho vya mabasi wanayofanyia kazi, na kwamba upekuzi utafanyika kwenye mageti yote kubaini wanaoingia na stendi na vitu hatarishi, sambamba na wageni wote wanaoingia kufanya kazi stendi kuhwkikisha wabasajiliwa.