26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MOURINHO AWEKA HISTORIA YA USAJILI WA PAUNI BILIONI 1

 

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, ameweka historia ya kuwa kocha wa kwanza kutumia pauni bilioni 1 (zaidi ya Sh trilioni 2 za Tanzania), kufanya usajili katika miaka 17 akiwa kocha katika timu mbalimbali barani Ulaya.

Mourinho anakuwa mbele ya Kocha wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti, ambaye ametumia pauni milioni 970 katika miaka 22 akiwa kocha pamoja na Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ambaye katika miaka tisa ametumia pauni milioni 859.

Guardiola ndio anaonekana kutumia fedha nyingi kwa sasa, baada ya kufikisha pauni milioni 200 za usajili baada ya kumsajili Kyle Walker na  Bernardo Silva, ingawa Mourinho amekuwa zaidi baada ya usajili alioufanya hivi karibuni.

United imetumia kiasi cha pauni milioni 75 kumsajili Romelu Lukaku, pauni milioni 40 iliyotumika kuinasa saini ya Nemanja Matic pamoja na pauni milioni 31 kumsainisha Victor Lindelof.

Nyota hao watatu wanamfanya Mourinho kutumia jumla ya pauni milioni 146 na kuwa chanzo cha kocha huyo kufikisha kitita cha pauni bilioni 1 alizotumia kusajili katika miaka 17.

Mourinho alifanya matumizi makubwa ya fedha msimu uliopita, ukiwa msimu wake wa kwanza katika klabu ya Manchester United, akiweka rekodi ya kutumia pauni milioni 89 ili kuinasa saini ya Paul Pogba, aliyesajiliwa akitokea Juventus.

Licha ya kocha huyo kufanya matumizi mbalimbali ya fedha, alitumia pauni milioni 33 kumsajili mchezaji wa zamani wa Tottenham, Luka Modric, wakati akiwa kocha wa Real Madrid.

Diego Costa alimfanya Mourinho kutumia kiasi cha pauni milioni 35, wakati Willian Borges da Silva, Cesc Fabreagas, Eric Bailly na Andriy Shevchenko kila mmoja akisajiliwa kwa gharama ya pauni milioni 30.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles