22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

MOURINHO AFICHUA ALIVYOICHINJA ARSENAL

LONDON, England


JUZI kocha Arsene Wenger na vijana wake wa Arsenal walishindwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Manchester United, mchezo uliokuwa wa 15 kwa kila timu tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu.

Mabao ya Man United katika mtanange huo yaliwekwa kimiani na Jesse Anthony, Valencia na Jesse Lingard aliyefunga mawili, huku lile la Gunners likipachikwa na straika wao raia wa Ufaransa, Alexandre Lacazette.

Hata hivyo, kocha Jose Mourinho amefichua siri ya kikosi chake kuondoka na pointi tatu licha ya kuwa ugenini, akisema wakati Arsenal wakiwa na mpira, vijana wake walihakikisha wanakaba vizuri na kuwasubiri wasogee ili wawatungue kwa ‘counter-attack’.

“Ndicho tulichokifanya. Ni kama ilivyotokea wakati (Romelu) Lukaku alipokutana uso kwa uso na Petr Cech. Lakini ukweli ni kwamba (Arsenal) wanaweza kusema walikuwa na nafasi lakini tulikuwa na kipa mzuri pia na nafikiri tulistahili ushindi,” alisema Mourinho.

Katika dakika ya 74 ya mtanange huo, nyota wake Paul Pogba alilimwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga beki wa Arsenal, Hector Bellerin, hivyo Mfaransa huyo atakuwa nje wakati Man United watakapokuwa Old Trafford Desemba 10, mwaka huu kuwakaribisha Man City.

Kabla ya mchezo huo, kesho Man United watakuwa nyumbani pia kumenyana na CSKA Moscow katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles