KATIKA kile kinachoonekana kutafuta nguvu ya mshikamano wa pamoja, Serikali ya Morocco imewasilisha ombi la kujiunga na Muungano wa Afrika (AU).
Morocco ilijitoa kwenye Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) miongo  mitatu iliyopita kutokana na mzozo wa umiliki wa sehemu ya Taifa la Sahara Magharibi.
Mzozo huo ulitokana na OAU kulitambua eneo hilo kama taifa huru, wakati Morocco ikilazimisha kuwa ni sehemu ya eneo yake
Kwa mujibu wa BBC, AU imetanabaisha kuwa Morocco imewasilisha rasmi ombi la kutaka kujiunga tena na muungano huo hivi karibuni.
Kwa mtazamo huo, duru zaidi zinaeleza kwamba Morocco kwa sasa inatambua kutokuwapo kwake kumepunguza ushawishi wake ndani ya Bara la Afrika.
Kwa mantiki hiyo kujiunga kwake  kwa mara nyengine na AU itasaidia kuipa nafasi zaidi ya kushawishi mataifa mengine kuunga mkono msimamo wake kuhusu sehemu ya Magharibi mwa Sahara.