32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Moduli ya kuwasilisha Rufaa za Zabuni Kieletroniki mbioni kuanza

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli ya mfumo mpya wa kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki (Complaint and Appeal Management) utaanza kufanya kazi rasmi kuanzia Julai 1, 2024.

Hayo yamebainishwa jana na Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Joto la Asubuhi cha Efm Jijini Dar es Salaam kuhusu Moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki.

“Mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, yameweka sharti la lazima kwa taasisi nunuzi na wazabuni kutumia Mfumo wa Kieletroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) ambapo PPAA kwa kushirikiana na PPRA tumejenga moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki ili kukidhi matakwa ya sheria,” amesema Sando.

Sando ameongeza kuwa moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kielektroniki itaanza rasmi Julai 1, 2024, ambapo pamoja na mambo mengine, amewasihi wazabuni na taasisi nunuzi wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Pwani kushiriki mfunzo ya awamu ya kwanza kuhusu mfumo huo Mei 29 na 30, 2024 jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles