PRODYUZA wa muziki kutoka Norway, Carl Hovind, amesema muziki wa Bongo Fleva hauandaliwi kwa ubora ndiyo maana unashindwa kuchezwa kwenye redio za Ulaya.
Carl alisema wasanii wengi wamewekeza kwenye video na kudharau audio za nyimbo zao ndiyo maana hazichezwi nchi zenye maendeleo katika muziki.
“Tatizo kubwa nililoliona Tanzania wasanii wanatumia fedha nyingi hata dola 20,000 kwa ajili ya kuandaa video za nyimbo zao nchini Afrika, lakini audio hawazigharamii,” alisema Carl.
Mtayarishaji huyo ambaye yupo nchini katika studio ya Diamond Platnumz, anatarajia kufanya kazi na wasanii wakubwa na wadogo.