29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mloganzila kufanya upasuaji wa matiti bila kukata ziwa

COSTANSIA MUTAHABA (DSJ) na TUNU NASSOR

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) – Mloganzila inatoa mafunzo kwa wataalamu wake kwa ajili ya kuanza kufanya upasuaji wa saratani ya matiti bila kuliondoa kwa watakaokuwa na dalili za awali.

Kwa kushirikiana na Kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya,  MNH imeandaa mafunzo hayo ya kisayansi kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji, tiba ya mionzi na dawa.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema lengo ni kukumbushana namna bora ya kuwapatia matibabu kwa njia 

ya kisasa wagonjwa ambao wamethibitika kuwa na saratani ya matiti.

“Mafunzo haya yanashirikisha wataalam 30 kutoka Muhimbili pamoja na Hospitali za rufaa nchini ambazo ni Bugando, KCMC, Mbeya na Hospitali binafsi ya Besta,” alisema.

Profesa Museru aliongeza kuwa  kupitia mtaalam mbobezi kutoka Nairobi, Kenya, Dk Peter Bird, wataalam hao watapatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa muda wa siku nne ambapo pia mada mbalimbali zinazohusu utoaji wa matibabu ya saratani ya matiti zitawasilishwa.

“Saratani ya matiti inachangia vifo kwa wanawake duniani kwa asilimia 25 hadi 35, pia ipo kwa kiwango cha juu katika nchi zilizoendelea kuliko nchi 

Zinazoendelea kutokana na wagonjwa kuchelewa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu.

“Kwa Tanzania saratani ya matiti niya pili kwa kusababisha vifo kwa wanawake ikiongozwa na saratani ya shingo ya kizazi, ambapo kati ya wanawake 20, mmoja yupo kwenye hatari ya kupata saratani hii ya matiti,” alisema Profesa Museru.

Profesa Museru alisema inakadiriwa kuwa asilimia 

80 ya wagonjwa wanaothibitika kuwa na saratani ya matiti nchini wanafika hospitali wakiwa katika hatua ya tatu na ya nne ya ugonjwa ambapo matibabu yake 

yanakuwa hayatoi matokeo mazuri.

“Pamoja na kutolewa kwa mafunzo haya, napenda kuchukua fursa hii kuzindua mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa wagonjwa wa saratani ya matiti kwa njia ya kielektroniki katika Hospitali ya Mloganzila, mfumo huu utarahisisha kuwa na takwimu sahihi ya 

wagonjwa na ufuatiliaji wa karibu wa matibabu yao,” alisema Profesa huyo.

Aliwashukuru Roche Pharmaceutical Company 

kwa kushirikiana na hospitali hiyo katika kuwajengea uwezo wataalam kwani watakaofaidika na mafunzo haya wataenda kuwajengea uwezo wataalam wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles