24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mlinzi wa Dk. Slaa aendelea kusota polisi

KangeziNa Asifiwe George, Dar es Salaam
KHALID Kangezi, mlinzi binafsi (PSU) wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi yake.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Camillus Wambura alisema uchunguzi unaendelea dhidi ya Kagenzi ambaye alifikishwa katika Kituo cha Polisi Osterbay juzi.
“Suala hili nilitakiwa kulitolea taarifa kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, lakini sikumpelekea kwa sababu uchunguzi haujakamilika.
“Bado tunaendelea kumchunguza mtuhumiwa, zipo taarifa mbalimbali ambazo hazijakamilika zitakapokamilika tutampelekea Kamishna Kova aweze kulizungumzia suala hilo.
“Tunaomba muwe na subira tuone itakuwaje na nitawasisitiza wapelelezi waongeze kasi ya uchunguzi tuweze kupeleka taarifa kwa Kamishna aweze kulitolea ufafanuzi katika jamii,” alisema Wambura.
Kangezi ambaye amekuwa mlinzi wa Dk. Slaa kwa miaka miwili, inadaiwa alikuwa akitumiwa na vyombo vya Usalama wa Taifa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuvujisha siri za chama hicho ikiwamo kupewa kazi ya kumuua Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
Hata hivyo, jana wanasheria wa Chadema waliitwa Kituo cha Polisi Osterbay kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles