24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mkwasa: Kila la heri ‘Cannavaro’

MKWASANA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, amemtakia kila la kheri aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, akieleza kuwa hawezi kumlazimisha kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Cannavaro alitangaza kuacha kuitumikia timu hiyo ya Taifa siku chache baada ya Mkwasa kumvua kitambaa chake cha unahodha na kumkabidhi nafasi hiyo mchezaji wa kimataifa Mbwana Samatta alipotwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Mchezaji huyo hakupendezwa na hatua iliyotumika kumvua unahodha huo, hivyo kutangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars, lakini wakati Mkwasa anaita kikosi wiki iliyopita kitakachovaana na timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ kwenye mchezo wa kirafiki, alimuita mchezaji huyo ambaye aliweka msisitizo kuwa hawezi kutengua maamuzi yake.

Akizungumza na MTANZANIA jana,  kocha huyo alisema kama ameendelea na msimamo huo, hawezi kumlazimisha zaidi anamtakia kila la kheri.

“Kuendelea kumlazimisha afanye kitu asichokitaka, ni sawa na kumlazimisha mbuzi kunywa maji kitu ambacho hakiwezekani kama kaendelea na msimamo wake huo namtakia kila la kheri na hilo nililihisi mapema ndio maana niliita wachezaji watano katika nafasi yake,” alisema.

Alisema kutokana na kukosekana kwake, hana haja ya kumuita mchezaji mwingine kuziba nafasi hiyo na atawatumia waliokuwepo.

Alisema wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume kwa baadhi ya wachezaji ambao tayari wameshajiunga kambini, ambapo wachezaji wa Yanga na Azam wataungana na wenzao leo.

Alisema kwa upande wa wachezaji wa kimataifa, wanatarajia kuwasili nchini Julai mosi kujiandaa na mchezo huo, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye mchezo wao wa kuwania tiketi ya kushiriki kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Misri, Juni 4 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles