25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

MKUU WA SHULE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA

Na HARRIETH MANDARI – GEITA


MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Kibumba iliyopo Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato mkoani Geita, Harun Musiba, ameuawa baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana.

Akizungumzia tukio hilo ambalo limethibitiswa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, mke wa marehemu, Mariam Kasholele, alidai mumewe alishambuliwa saa 5 usiku wakati akitoka kuangalia mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC ya Tanzania na URA ya Uganda.

Alisema tukio hilo limetokea Januari 13, mwaka huu, na kwamba mumewe inadaiwa baada ya kukaribia mlango wa kuingia ndani, alivamiwa na watu wasiojulikana ambao walimshambulia.

“Tulisikia kishindo upande wa mlango wa kuingilia nyumbani, baada ya kutoka na kuangalia kinachoendelela, nilimwona mume wangu akiwa amelala chini ila nilidhani ameanguka kutokana na kulewa.

“Baada ya kuangalia kwa makini nilishuhudia akiwa ametapakaa damu kutoka kwenye majereha kadhaa mwilini mwake,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, alipiga kelele kuomba msaada, lakini watu walipofika tayari alikuwa amepoteza uhai.

Naye Kamanda Mwabulambo, alisema wameanza uchunguzi wa tukio hilo.

Mwili wa marehemu, umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Chato, ukisubiri taratibu za mazishi ambayo yalipangwa kufanyika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles