25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mkuu wa chuo apandishwa kizimbani

Chuo cha Uhasibu Njiro
Chuo cha Uhasibu Njiro

NA JANETH MUSHI, ARUSHA

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Njiro (IAAA), Johannes Monyo na wenzake kumi, wamepandishwa kizimbani jana kwa kosa la kutumia vibaya madaraka na kuisababishia Serikali hasara.

Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kilongozi Adam, alidai mahakamani hapo kuwa mkuu huyo alitumia madaraka yake vibaya kinyume na kifungu cha 31 cha sheria no 11 ya TAKUKURU.

Kilongozi ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha manunuzi chuoni hapo, aliwataja watuhumiwa wengine katika shauri hilo namba 33 la mwaka 2014 kuwa ni Jerome Agustine, Faraji Mnyepe, Chacha Wambura, Mpoki Mwasaga na Papias Njaala.

Wengine ni Mathew Melita, Mary Thomas, Elisaria Kisanga, Gerald Malisa na Honory Mkelemi ambao wote ni wafanyakazi katika chuo hicho kilichopo eneo la Njiro, nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Akisoma mashtaka yanayowakabili, Kilongozi alidai kuwa shitaka la kwanza linamkabili Monyo na Agustine wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao ambapo Septemba 30, 2011, watuhumiwa hao walibadilisha matumizi ya zaidi Sh milioni 6 na kujinufaisha nazo binafsi.

“Wametumia madaraka yao vibaya kwani fedha hizo zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa “Solar Power Back up Kit” lakini walibadilisha matumizi ya fedha hizo na Monyo kujipatia manufaa binafsi,” alidai mahakamani hapo.

Katika shtaka la pili linalowakabili watuhumiwa 10 isipokuwa mkuu huyo wa chuo kwa pamoja wakiwa wajumbe wa bodi ya manunuzi chuoni hapo

walitumia madaraka yao vibaya kwa kuidhinisha matumizi ya fedha hizo kwa utaratibu wa “single source” kinyume na sheria ya manunuzi ya umma.

Alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao kati ya Novemba 1, 2011 na Novemba 30, 2011, walisababisha kampuni ya Helvetic Solar Contractors kujipatia fedha isiyo halali na kuisababishia Serikali hasara.

Shtaka la tatu linalowakabili Augustine, Mnyepe na Mkelemi, washitakiwa hao wanadaiwa kuwezesha mchakato wa malipo ya zaidi ya Sh milioni sita kwa kampuni ya Helvetic Solar Contractors kinyume cha Sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2005.

Aidha katika shauri hilo washitakiwa watatu hawakuweza kufika mahakamani hapo ambao ni Mpoki Mwasaga, Mathew Melita na Gerald Malisa na mwendesha mashitaka wa Serikali aliiomba Mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa washitakiwa hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles