25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MKUTANO WA TRUMP, KIM JONG-UN WAANZA KUANDALIWA

SEOUL, KOREA KUSINI


UJUMBE wa Korea Kusini umeanza maandalizi ya mkutano wa kihistoria baina ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un.

Ujumbe huo wa viongozi wa Korea Kusini unatarajiwa kufika China na Japan kutoa maelezo juu ya mkutano huo ambao muda na mahali bado hapajajulikana.

Wiki iliyopita, viongozi hao walifikisha ujumbe kwa Rais Trump juu ya kukutana na kufanya mazungumzo na Kim Jong Un, ambapo alikubali mara moja na kuzipa taarifa China na mshirika wake Japan.

China imeonesha nia ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo lakini mahala pengine pa kufanyika mkutano huo pametajwa kuwa huenda ikawa Uswisi, Sweden au Panmunjom (Korea Kaskazini).

Licha ya kupongeza mkutano huo, wakosoaji wa siasa za Marekani wameonya iwapo mazungumzo hayo yataenda vibaya  nchi hizo mbili zitakua na uhusiano mbovu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles