24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Jamii Forum akutwa na hatia

Kulwa Mzee -Dar es salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo kutumikia kifungo cha mwaka mmoja au alipe faini ya Sh milioni tatu kwa kosa la kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa taarifa kwenye mtandao wa Jamii Forum.

Melo alitiwa hatiani jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupatikana na hatia ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa taarifa mbili zilizotumwa kwenye mtandao wa Jamii Forum ambazo zilikuwa zinahusu Kampuni ya Oilcom.

Mahakama hiyo imemwachia huru mwanahisa wa mtandao huo, Micke William kwa sababu hausiki moja kwa moja na mtandao huo.

Hata hivyo, Melo aliachiwa huru baada ya kulipa faini.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Simba alisema upande wa mashtaka ulileta mashahidi wanne ambao ni askari polisi waliokuwa wakifanya uchunguzi kuhusu kesi hiyo.

Alisema mashahidi hao watatu waliandika barua kwenda  Jamii Forum kuomba kupatiwa maelezo kuhusu taarifa hizo mbili, lakini mtandao huo kupitia Kampuni ya Uwakili ya Victory Consultant walidai wako tayari kutoa ushirikiano, lakini walipaswa kuelezwa ni kifungu gani cha sheria kinachowataka kutoa taarifa za wateja wao.

Hakimu Simba alisema baada ya upande wa mashtaka  kufunga ushahidi, washitakiwa hao walikutwa na kesi ya kujibu na kwamba watajitetea wenyewe.

Alisema Melo katika utetezi wake alikubali kuwa miongoni mwa wakurugenzi wa Jamii Forum na kwamba alikana mashitaka hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles