23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mkitekeleza siasa kwa mwonekano unaoendana na jamii, malalamiko haya yataishia mbali

FARAJA MASINDE

SERIKALI iko kwenye hatua za mwisho kabisa kuhamia kwenye mfumo wa manunuzi ya umma kwa njia ya mtandao (TANePS) ambao kwa kiasi kikubwa utaondoa usumbufu ambao ulikuwa unajitokeza awali.

Mfumo huu siyo tu kwamba utaokoa usumbufu, bali pia utasaidia kuepusha uwapo wa mianya ya rushwa ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye michakato ya manunuzi hapa nchini.

Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA), imeona umuhimu wa kuhama kwenye mfumo wa manunuzi unaotumika hivi sasa unaohusisha nyaraka kwa kiasi kikubwa na kuhamia kwenye mfumo mpya wa TANePS.

Awali, kulikuwapo ucheleweshwaji wa makusudi kwenye manunuzi mbalimbali. Pia ilikuwa ni changamoto kwenye utoaji wa zabuni jambo ambalo lilitengeneza mazingira ya giza na hata kujenga vimelea vya rushwa.

Hivyo, hii ni hatua nzuri ambayo imeweza kufikiwa na serikali katika kuhakikisha kuwa masuala yake mengi yanafanyika kwa njia ya mtandao kama ilivyo kwenye mataifa yaliyoendelea, kwani bila kumung’unya maneno jambo hili litaondoa ubabaishaji ambao ulikuwa ukijitokeza mara kwa mara ikiwamo ucheleweshaji wa makusudi.

Hadi sasa taasisi za manunuzi ya umma 418 zimejisajili kwenye mfumo huo kati ya 540 sawa na asilimia 77.4. Hii inatia matumaini kuona kuwa taasisi nyingi zimeunga mkono mpango huo wa serikali wa kuhakikisha kuwa mambo mengi yanafanyika kisasa zaidi na hivyo kusaidia kunyanyua uchumi kwa kiasi kikubwa, kuokoa gharama na hivyo kupata huduma kwa haraka.

Kama hiyo haitoshi serikali imeweka bayana kuwa kuanza kutumika kwa mfumo huo wa TANePS utaokoa kiasi cha Sh bilioni 34 kwa muda wa miaka mitano ya kwanza.

Hii ina maana kuwa kiwango hicho cha fedha kitaelekezwa kwenye miradi mingine ya kiuchumi ambayo kwa namna yoyote itakuwa na manufaa kwa nchi.

Sasa basi, ni vema taasisi zote husika zilizosalia zikajiunga na mfumo huu kabla ya Desemba 31, mwaka huu, ili kurahisha mkakati wa serikali.

Lakini pia serikali iende mbali zaidi kwa kuangalia namna gani masuala mengi zaidi yatafanyika kwa njia ya mtandao ili kuokoa gharama zisizo za lazima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles