27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MKEMIA MKUU AWAONYA WAFANYABIASHARA WA KEMIKALI


Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, amesema mtu yeyote atakayeuza kemikali ni lazima amuuzie yule aliyesajiliwa kwa kuwa sheria inaagiza kila anayehusika na kemikali lazima awe amesajiliwa

Profesa Manyele alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua mafunzo ya wauzaji, wasafirishaji, wahifadhi na watumiaji wa kemikali katika Kanda ya Kati Dodoma.

Kwa mujibu wa Profesa Mnyele, anayeleta athari katika suala la kemikali ni mtumiaji wa bidhaa hiyo na asiyefuata taratibu.

“Wafanyabiashara mnaotumia kemikali mmeingia kwenye hatua ya juu, tuwaombe sana hizo shughuli zenu msije mkathamini biashara zenu mkasahau afya za Watanzania na mazingira yetu.

“Kwa yeyote anayekiuka taratibu za biashara hiyo, ataadhibiwa kwa kuzingatia kiwango cha mtaji wa biashara yake.

“Kwa hiyo, nawaomba muwe mnazingatia hii sheria kwa kuwa kemikali nyingi zilikuwa zinaingia nchini kiholela na watumiaji wengi walikuwa wanaingiza kiholela.

“Katika ufanyaji wa biashara hii, Serikali inasisitiza kufuata sheria bila shuruti na kufuata taratibu zilizoainishwa kisheria.

“Wapo watu ambao wamekuwa wakifanya shughuli hii kwa siku nyingi, lakini hawajapata usajili.

“Udhibiti wa biashara hiyo kwa sasa ni wa kiwango cha juu tangu sheria hii ianze kutumika ndani ya miaka 13 na sasa tumeweka mifumo ya udhibiti,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo, mkemia mkuu huyo alisema ni muhimu kwa kuwa mbinu za matumizi ya kemikali zinabadilika kulingana na mazingira pamoja na wakati.

Naye Mshiriki wa mafunzo hayo, Neema Lusekelo kutoka Kiwanda cha Tumbaku cha mjini Morogoro, alisema mafunzo hayo yatawasaidia kujua matumizi sahihi ya kemikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles