23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mkapa: Wapumbavu… malofa

1Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani hapo, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na Tanu, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuiomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Alisema kati ya wagombea urais wanane waliopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), hakuna mwingine mwenye sifa nzuri kama Dk. Magufuli.

Katika hatua nyingine, alisema haitoshi kuchukia umaskini bali inatakiwa mtu aeleze ni namna gani ataweza kupambana na tatizo hilo.

“Eleza ni kwa namna gani utapambana na umasikini, ilani ya CCM inaonyesha namna ya kutekeleza kama alivyofanya Dk. Kikwete,” alisema Mkapa.

Aliwataka wanachama wa CCM kuwashawishi Watanzania kuipigia kura CCM ili kuendeleza ukombozi wa maendeleo ya Tanzania na ushindi ni lazima kwa CCM.

Mwinyi: Wao ni CCM B

Kwa upande wake Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, naye aliwarushia vijembe wapinzani kwa kusema kuwa ni CCM B na kwamba hakuna sababu ya kuwachagua kwa sababu CCM A ipo.

“Wanaohama wenyewe wamesema kwa nini wanaenda huko, siyo mimi ninasema, wanasema wanaenda kuwafundisha namna ya kuioandoa CCM, kwa hiyo dhamira inayowapeleka huko ni kutafuta namna ya kuishinda CCM hali iliyosababisha kutengeneza CCM mbili ambazo ni A ya kwetu na B ni ile ya upinzani mliyoisikia wenyewe, kama A ipo B ya kazi gani?,” alihoji Mwinyi.

Warioba: Magufuli ni mzalendo

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, alisema sababu za ufisadi ni viongozi kuwa karibu na matajiri.

“Miaka 20 iliyopita Mkapa alinipakazi ya kuangalia ufisadi, katika taarifa ile tulisema chanzo cha ufisadi ni viongozi kuwa jirani na matajiri, ‘mmewahi kumwona Magufuli yupo karibu na matajiri?  “hapanaa”, wananchi walijibu.

Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema Magufuli ni mzalendo hasa kwa nchi yake akiwa pamoja na mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan.

Alisema pia kwamba, Dk. Magufuli amechaguliwa na chama chake kumetokana na mgombea huyo kuwa na sifa za uadilifu, uchapakazi na uzalendo.

“Mkutano mkuu ulisikiliza maombi ya wana CCM waliokuwa wengi wakimtaka mgombea wao awe mwadilifu, mzalendo na mchapakazi,” alisema Warioba.

Alisema kumekuwa na ufisadi mwingi serikalini ikiwa ni pamoja na Escrow, Richmond, Operesheni tokomeza na Epa, lakini Dk Magufuli hajawahi kukumbwa na kashfa yoyote katika sekta ya ujenzi.

“kila alipokwenda iwe ardhi au uvuvi amekuwa akipita kwa wananchi na kuwaeleza kuhusu kazi zao, ikiwamo na kuwa mkali kwa kuwa hataki kazi za ovyo ovyo,” alisema.

Dk. Sheni: Tutawanyoa pande mbili 

Kwa upande wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohammed Shein, alisema Wazanzibari wapo pamoja na Dk. Magufuli kama ambavyo waliwaunga marais wengine waliopita.

Hata hivyo Dk. Sheni alisema ushindi wa CCM uko wazi huku akijigamba kuwa vyama vya upinzani haviwezi kufurukuta kwa upande wa Zanzibar.

Alisema kuwa sababu za kumuunga mkono zinatokana na historia ya nchi hizi katika suala la muungano kwa kuanzishwa na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume kwa kuanzisha Tanzania.

“Kwa kuendeleza undugu wetu wa damu tutahakikisha Dk. Magufuli na Suluhu kushinda katika uchaguzi ujao kwa kasi na ari ile ile kama iliyokuwa kwa Rais Kikwete,” alisema.

Alisema kuwa CCM ndicho chama chenye wagombea wenye sifa za kuiletea Tanzania maendeleo kama yale yaliyofanywa na wagombea waliopita katika awamu zilizopita.

Aliwataka wana CCM wasijaribu kutoa uongozi wa nchi kwa kujaribu kwa sababu suala la dola halijaribiwi kama wengi wanavyofikiri  hivyo msitoe uongozi kwa wapenda sifa na wasiokuwa na sifa.

“Kwa upande wa Zanzibar wembe ni ule ule. Tutawanyoa pande mbili hatuachi panki na nyinyi huku (bara) wanyoweni,” alisema Dk. Sheni.

Makongoro: Sumaye ni mwongo

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Makongoro Nyerere amemwita waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kuwa ni mwongo.

Makongoro alisema kuwa sababu kubwa ya uongo wa Sumaye ni kusema kuwa angechaguliwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM angehama chama.

“CCM imefuata ushauri wake na kumuondoa sasa amehama hivyo atakuwa kasema kweli? na mtu asiyesema kweli ni nani?,” alihoji na wananchi wakasema ‘mwongo’.

“Sisemi mimi ila mmesema Sumaye ni mwongo kwa sababu ndiye aliyetushauri tusimpatie chama Lowassa huku akisema tukimpatia chama atahama lakini pamoja na kumng’oa amekimbia huyu mtu atakuwa hakusema kweli,” alisema.

Watu 10 wazimia Jangwani

Hata hivyo watu zaidi ya 30 jana walipoteza fahamu kwa kukosa hewa kwenye mkutano huo wa kampeni uliofanyka katika viwanja vya Jangwani.

Katika banda la msalaba mwekundu MTANZANIA lilishuhudia wanawake, vijana na watoto wakiwa wamelazwa chini wakipewa huduma ya kwanza.

Katika huduma hizo, gari la kutoa huduma vijijini ‘mobile clinic’ likiwa na madaktari na wahudumu wa afya lilikuwa likitoa huduma huku lile la wagonjwa likizunguka na kuchukua waliohitaji huduma zaidi za matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles