24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mjiandae kisaikolojia mnaotaka Umeya wa Jiji la Dar- JPM

Na Brighter Masaki, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua Manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadhi na kuwa Jiji, lengo likiwa ni kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Dk. Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Februari 24, 2021. wakati akizindua Daraja la Juu la Ubungo lililopewa jina la Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Balozi John Kijazi.

“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndiyo iwe Jiji, itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa.

“Tunataka Manispaa moja katika Jiji la Dar es Salaam ndiyo ipandishwe hadhi iwe Jiji halafu nyingine ziwe Manispaa, Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa maana ndiyo ipo katikati, Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Dk. Magufuli.

Aidha, ametoa angalizo kwa wanaojindaa kuwania nafasi za Umeya; “Wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa Jiji la Dar es Salaam na hawana maeneo wajue hicho kimekwisha, tunataka Manispaa moja ya Jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe Jiji halafu nyingine ziwe Manispaa, kama kwenye Majiji mengine, mjiandae kisaikolojia waliokuwa wanataka Umeya wa Dar.

“Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na nafikiri Ilala inafaa kuwa Jiji kwa sababu ndio katikati ya Mji, Ubungo itasubiri kidogo kwa kuwa hata Barabara bado hazijatengenezwa, lazima tuijenge Dar es Salaam ya kisasa, liwe Jiji kweli la kisasa.

“Haiwezekani unakuwa na madiwani wamekaa tu wanatengewa bajeti hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya barabara hayo ni matumizi bora ya fedha za walipakodi kwa hiyo mjiandae kisaikolojia meya atapatikana katika manispaa ya Ilala. Waziri Jafo ameshaniletea drafti nadhani nikimaliza ziara nitaenda kusaini,” amesema Dk. Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles