29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Miundombinu iliyoharibiwa na mvua Ilala yaanza kukarabatiwa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kukarabati barabara zilizoharibiwa na mvua ili ziweze kutumika kama awali.

Miongoni mwa barabara hizo ni ile inayounganisha Mtaa wa Kichangani na Mtaa wa Kinyerezi ambayo iliathiriwa na mvua na kusababisha karavati kusombwa na maji.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa karavati katika barabara inayounganisha mitaa ya Kichangani na Kinyerezi.

Akikagua ukarabati wa barabara hizo Desemba 18, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludugija, amesema mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha uharibifu wa barabara na madaraja katika baadhi ya maeneo.

“Nimelazimika kufika hapa na wataalam ili kuona kazi inavyoendelea, tumejipanga kuhakikisha pamoja na mvua hizi zinazoendelea makusudio yetu ni kuona barabara hii zinarudi katika hali yake,” amesema Ludigija.

Aidha amemuagiza mkandarasi anayekarabati barabara hiyo kuongeza kasi ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao.

Mkuu huyo wa wilaya pia alitembelea eneo la Kifuru ambako barabara inyounganisha mtaa huo na maeneo mengine kama ya Bangulo na Gongolamboto imekatika na kuwaagiza wataalam kufanya usanifu wa haraka na kumpata mkandarasi ili kujengwe karavati kubwa litakaloweza kupokea maji.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, akiangalia athari zilizosababishwa na mvua katika barabara inayounganisha eneo la Kifuru na maeneo mengine ya wilaya hiyo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah Mgitu.

Naye Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga, amesema katika eneo la Kichangani wamefanya tathmini na kubaini karavati lililokuwepo lilikuwa dogo na mvua zilikuja na uchafu mwingi hivyo wataweka karavati kubwa lenye kipenyo cha mita 1.2 tofauti na lile la awali liilokuwa na kipenyo cha 0.6.

“Tumechukua hatua za haraka na tumempa mkandarasi siku tano awe amekamilisha kazi, tutamsimamia usiku na mchana kuhakikisha mawasiliano yanarejea kama kawaida,” amesema Mkinga.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah Mgitu, amesema kukatika kwa barabara hizo kumesababisha kukosa mawasiliano ya mitaa na kuathiri upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii.

Nao baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wameiomba Serikali ijenge makaravati makubwa ili yaweze kudumu na kuwasaidia kwa kipindi kirefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles