Tume ya uchaguzi nchini Misri imetangaza leo kwamba kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba ikiwemo uwezekano wa kumruhusu rais Abdel-Fatah al sisi kubakia madarakani mpaka mwaka 2030,itafanyika Aprili 20-22.
Tangazo la tume hiyo limekuja baada ya hapo jana bunge la Misri kuidhinisha mageuzi ya katiba ambayo yatamruhusu rais el-Sisi kuendelea kujiimarisha madarakani. Maafisa wa Misri wanajaribu kuzuia kuongezeka kwa malalamiko yanayotolewa katika mtandao yakipinga mageuzi hayo.
Bunge lenye wajumbe 596 linalohodhiwa na wafuasi wa el-Sisi lilihitaji wingi wa thuluthi mbili tu ya kura kupitisha mageuzi 14 na kuingiza vipengee vingine vingi vipya.