23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MIPANGO YASUKWA MKUTANO MKUU TFF

Jamal Malinzi
Jamal Malinzi

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MKUTANO Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unatarajiwa kufanyika Februari 20, mwakani katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, huku kukiwa na ajenda ya kufanya mabadiliko katika katiba ya shirikisho hilo.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kufanyika kutokana na mapendekezo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuridhia.

Mkutano huo unafanyika huku vuguvugu la mchakato uchaguzi mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwakani, likiwa linazidi kupamba moto.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za uhakika kutoka Fifa ambazo zimelifikia MTANZANIA jana, shirikisho hilo limepanga kushawishi wajumbe kukubali kupunguza idadi ya wajumbe watakaopiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwakani kutoka wanne hadi wawili.

Fifa imethibitisha kupitia baruapepe kuwa ipo tayari kugharamia mkutano huo kwa kuanza kufanya matayarisho ya ukumbi katika Hoteli  ya Serena.

Mapendekezo ya kutaka kupunguza wapiga kura kwenye uchaguzi ujao wa TFF yaliwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Desemba mwaka jana jijini Tanga, lakini ajenda hiyo iliwekwa kiporo.

“Kama wajumbe watakubali kupitisha mapendekezo haya ina maana katiba ya TFF itabadilishwa ili kupunguza idadi ya wajumbe ambao watapiga kura katika uchaguzi ujao wa Oktoba,” kilieleza chanzo hicho.

Hata hivyo, wajumbe wanaotarajia kuhudhuria mkutano huo wameanza kugawanyika kwa baadhi kupinga kufanyika kwa maboresho ya katiba ya TFF huku wengine wakiunga mkono kwa kutaka yafanyike baada ya uchaguzi wa mwakani.

Wajumbe hao wanadai kuwa vyama mbalimbali vya soka tayari vimefanya uchaguzi na kupata wawakilishi wao, hivyo hakuna sababu ya kufanyika maboresho ya katiba kuelekea uchaguzi ujao.

Pia wajumbe wa Fifa wanatarajia kutua nchini wakati wowote ili kukamilisha maandalizi ya mkutano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles