29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Minziro apuuza ushindi wa Julio

RAMADHAN HASSAN, DODOMA

KOCHA wa timu ya Arusha United, Fred Minziro, amesema kipigo walichokipata kutoka kwa Dodoma FC hakijawafanya wapoteze mwelekeo, badala yake kimewafanya wajipange upya ili kuhakikisha wanashinda michezo ijayo.

Arusha United ilikumbana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Dodoma katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza uliochezwa juzi Uwanja wa Jamhuri,  Morogoro.

Kipigo hicho kimeifanya Arusha United iliyoko kundi B, kusaliwa na pointi 14 wakati Dodoma FC ikifikisha pointi 14, huku Boma ikiendelea kukalia uongozi na pointi zake pointi 17.

Akizungumza baada ya pambano hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, kumalizika, Minziro alisema amekukubaliana na matokeo na sasa anajipanga  kisawasawa kwa ajili ya mchezo unaofuata.

“Japo namlaumu mwamuzi wa mchezo kwa kutokufuata sheria kwa kuipendelea Dodoma FC, lakini nakubaliana na  matokeo na najipanga kwa mchezo ujao,” alisema.

Minziro ambaye amewahi kuzichezea timu kadhaa miaka ya nyuma, ikiwemo Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, alisema anaamini kikosi chake kitavuna pointi tatu katika mchezo wao unaofuata dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, licha ya kwamba watakuwa ugenini.

“Hili limeisha, sasa macho yetu na akili zetu tunayapeleke Tabora, malengo yetu ni yale yale kucheza Ligi Kuu,” alisema.

Kwa upande wake, Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo, aliwashukuru wachezaji wake kwa kupambana na kupata ushindi.

“Niliwambia na naendelea kuwaambia tulijipanga kushinda na tumeshinda, sasa tunaenda kucheza mechi tano mfululizo ugenini, hii ratiba tumwachie Mungu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles