22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mimi siangalii Kabila-Rais Samia

NA MWANDISHI WETU

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema anakotoka hakuna makabila na katika utendaji kazi haangalii kabila la mtu, lakini kuna watu wanapofanya makosa wakishikwa wanasema wanawajibishwa kutokana na kabila fulani.


Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2021 wakati akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.


“Niko hapa bila kuangalia kabila flani, sasa watu wanafanya makosa ukiwashika ukiwawajibisha wanasema nimewajibishwa sababu wa kabila flani, sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia Mzanzibar, sina kabila na kwa maana hiyo hata kwenye utendaji wangu wa kazi sina kabila.

“Uwe mmakonde, uwe mnani ukikosea kwenye kazi mimi na wewe wala sitakufumbia jicho, sasa kama umetoka ulikotoka ukitumbuliwa useme mimi wa kabila fulani hapana, hiyo sumu mnaipeleka sana na naomba isimame, Samia Suluhu mimi sina kabila.

“Mwalimu Nyerere alitufundisha kufanyakazi bila kuangalia makabila ya watu na ndicho tunachokifanya, kwa hiyo muende mkafanye kazi zenu, msifanye kazi mkafanya mambo yasiyofaa mkishikwa mnasema sababu mimi ni wakabila flani, mimi siangalii kabila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles