28.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mimba zapungua shuleza msingi, sekondari

Nyemo Malecela Kagera

TATIZO la mimba limepungua kutoka 201 mwaka jana hadi  65  Novemba, mwaka huu ambayo ni asilimia 68 kwa shule za msingi na sekondari mkoani Kagera.

Takwimu hizo, ziltolewa na Ofisa Elimu Mkoa wa Kagera, Juma Mhina wakati wa kikao cha wadau wa elimu cha mjini  Bukoba jana.

Alisema ufuatiliaji na upimaji unaendelea kwenye shule zote za sekondari na msingi ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za uthibiti wa mimba kila robo ya mwaka.

Alisema kwa mwaka 2018 katika Wilaya ya Biharamulo kulikuwa na kesi za mimba 16 (tatu shule ya msingi na 13 sekondari) ambapo kwa mwaka huu wilaya hiyo haina kesi yoyote ya mimba. 

“Halmashauri ya Bukoba ilikuwa na kesi za mimba 30 (kesi nane za shule za msingi, 22 za sekondari) ambapo mwaka huu kiwango hicho kimeshuka na kufikia kesi 11, tatu za shule ya msingi na nane sekondari.

Kwa mwaka 2018 Bukoba Manispaa shule ya msingi haikuwa na kesi ya mimba bali sekondari ilikuwa na kesi nne na mwaka huu Halmashauri hiyo ina kesi 14, msingi moja na sekondari 13,” alibainisha.

Kwa upande wa Wilaya ya Karagwe Mhina alisema kulikuwa kuna mimba 10, kwa shule za msingi mimba nne na sekondari mimba sita. Na kuwa kwa sasa kuna mimba mbili,  moja kwa shule ya msingi na moja kwa shule ya sekondari.

Alisema Kyerwa kulikuwa na mimba saba, moja kwa shule za msingi na sita kwa sekondari. Na sasa wilaya hiyo ina kesi ya mimba mbili zote za shule za sekondari.

“Kwa mwaka 2018, Wilaya ya Misenyi kulikuwa na kesi 17 za mimba, shule ya msingi tisa na sekondari nane. Na sasa wilaya hiyo ina kesi za mimba tisa ambapo mimba mbili ni kwa shule za msingi na saba kwa shule za sekondari.

Kwa upande wa Muleba kulikuwa na kesi za mimba 80, kesi za mimba 20 kwa shule ya msingi na 60 kwa sekondari. Kwa sasa zipo kesi 11, kesi tatu za shule za msingi na nane kwa sekondari,” alieleza.

Kwa Wilaya ya Ngara mwaka 2018 kulikuwa na kesi za mimba 37 ambapo shule za msingi kulikuwa na kesi 12 na sekondari 25. Kwa mwaka huu wilaya hiyo imekuwa na kesi za mimba 16, kwa shule za msingi kukiwa na kesi nne na sekondari kesi  12.

Mhina alisema ukiondoa Bukoba Manispaa ambayo takwimu imepanda kutoka mimba nne (2018) hadi mimba 14 (2019), Halmashauri zilizosalia takwimu za Mimba zimeshuka.

“Ufuatiliaji unaendelea kufanyika na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria wanaohusika,” alisema.

Mwisho

Jaji Kiongozi aimwagia sifa mahakama

Na  Mwandishi  Wetu

JAJI Kiongozi wa Mahakama  Kuu  ya Tanzania,Dk. Eliezer Feleshi ameupongeza  uongozi  wa  Mahakama  Kuu Kanda ya Tanga kwa kazi kubwa  waliyoifanya  ya utekelezaji wa Mahakama Mtandao (E- Judiciary), licha  ya kupata bajeti ndogo.

Dk. Feleshi alimpongeza Ofisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Amina Ahmad kutokana na jitihada zake za kutumia vyema taaluma yake kubuni na kuanzisha mifumo ya kielektroniki ya ndani kwa ajili ya kusaidia utunzaji na uhifadhi salama wa majalada ya mashauri na nyaraka mbalimbali za kiutendaji.

Ofisa alibuni mifumo hiyo  kupitia mifumo ya “Tanga Record Centre”, E- Office, E-Library na Receive & Return File Database (Double R).

Pia alimpongeza kwa kuwezesha kusimikwa mifumo ya matangazo kwa umma na uoneshaji wa orodha ya mashauri kwenye televisheni.

Alipongeza utendaji wa pamoja uliojengwa na watumishi wa Kanda ya Tanga chini ya uongozi na usimamizi wa Jaji Mfawidhi, Amiri Mruma.

Dk. Feleshi aliyasema hayo, baada ya kupokea taarifa ya kanda iliyosomwa kwake na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanga, Francis Kabwe na baadae kujionea shughuli na utendaji wa mifumo ya kielekroniki kupitia ratiba ya ziara yake ya siku moja aliyoifanya tarehe 10 Desemba mwaka huu.

Katika ziara hiyo  alionyesha kuridhishwa na utendaji wa kanda hiyo na kusema  inastahili kimkakati kwa mafunzo ya vitendo kwa viongozi wapya  kwa kuzingatia iko jirani na Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA).

Aliutaka uongozi kuwatambua, watumishi wanaothubutu kuonesha ubunifu kutokana na vipaji vyao waeleweke na kuenziwa ili waendelee kuwa hazina ya mhimili wa mahakama, badala ya kukatishwa tamaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles