22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Watakiwa kuchangamkia uandishi wa insha

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amewataka wakuu wa shule kuwashawishi wanafunzi kuchangamkia fursa za mashindano ya uandishi wa insha za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kauli hiyo, aliitoa jijini hapa jana, wakati wa hafla ya kutunuku vyeti kwa washindi wa kitaifa wa shindano la uandishi wa insha za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Alisema uandishi wa insha, utawasaidia  na kuwaongozea wanafunzi uwezo wao kukuza ujuzi wa lugha.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wakuu wa shule  kuwashawishi wanafunzi kuchangamkia fursa za mashindano hayo.

“Napenda kusisitiza wakuu wote wa shule kuendelea kuwashawishi wanafunzi kuchangamkia fursa za mashindano pamoja na kuwaongozea uwezo wao kukuza ujuzi wa lugha,uandishi wa insha unaongeza maarifa kwa ujumla,”alisema

Aliwataka kusimamia kwa umakini mchakato wa mashindano hayo ili kuhakikisha ushiriki wa wanafunzi wengi.

“Namwaagiza kila mkuu wa shule kuteua mratibu atakayefanya kazi ya kusimamia wanafunzi ili wazingatie na kufuata taratibu zote za uandishi wa insha ili tuweze insha nzuri na kuziwasilisha katika mashindano ya kanda,”alisema.

Mratibu wa shindano hilo,Sylvia Chinguwile alimtangaza, Vanessa Lema kutoka Shule ya Sekondari Longodo mkoani Arusha  ambaye yupo kidato cha nne kuwa mshindi.

Wengine walioshinda, ni Thomas Kalisha mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Kibasila, Dar es salaam ambaye alishika nafasi ya pili,huku nafasi ya tatu ikishikwa na Monica Nyamhanga  wa Shule ya Sekondari Heritage ya mkoani Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles