23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 50/- kila kijiji kuanza mwaka 2016/17

Antony MavundeNA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

SERIKALI imesema itaanza kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipa kila kijiji nchini Sh milioni 50  katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Sera, Uratibu, Bunge la Walemavu, Antony Mavunde alipojibu swali la  Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.

Bulembo alitaka kujua   ahadi ya Sh milioni 50 kwa kila kijiji itatekelezwa lini.

Mavunde alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kila kijiji kupewa Sh milioni 50 itaanza kutekelezwa  katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.

Alisema utaratibu wa kugawa fedha hizo unaandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

‘’Pamoja na mikakati yote hiyo vigezo ambavyo vimekuwa vikitumika katika kutoa mikopo  na mitaji  kwa vijana ni umri usiozidi miaka 35 ambavyo  ni kujiunga na Saccos za vijana za wilaya na kuunda vikundi na kuvisajili kisheria,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha vijana wanakuwa wajasiriamali na wanaweza kupatiwa mikopo na mitaji, serikali imejiwekea mikakati ya kutambua vijana na mahitji yao katika ngazi mbalimbali  na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali ya vijana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles