MAREGESI PAUL Na RAMADHAN HASSAN -DODOMAÂ Â Â Â Â Â Â |Â Â Â Â
MAWAZIRI wa zamani watano wametajwa katika ripoti ya moja ya kamati mbili maalumu za Bunge zilizoundwa kuchunguza masuala ya uvuvi bahari kuu na yale ya gesi asilia nchini, kwa kuingia mikataba mibovu inayodaiwa kuisababishia hasara Serikali.
Waliotajwa ni Daniel Yona, Maokola Majogo, marehemu Abdallah Kigoda, Nazir Karamagi na William Ngeleja ambao wote kwa vipindi tofauti waliwahi kuhudumu katika iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini.
Mawaziri hao wa zamani walitajwa jana wakati kamati hizo zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, zilipowasilisha ripoti zao nje ya ukumbi wa Bunge jijini hapa.
Kutajwa kwa Ngeleja, Yona na Karamagi, ni mwendelezo wa kashfa ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yao mara kadhaa sasa.
Kwa upande wake, Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema kupitia CCM, hii ni mara ya tatu kutajwa kwenye kashfa.
Mara ya kwanza alihusishwa na ufisadi wa fedha za Escrow, akinufanika na mgawo wa sh milioni 40.4 ambazo baadae alizirudisha.
Alitajwa pia katika ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza mfumo wa uchimbaji, udhibiti, usimamizi na umiliki wa madini ya almasi na Tanzanite, akidaiwa kuhusika na dosari zilizoisababisha nchi kupoteza fedha nyingi.
Yona ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa awamu ya tatu, amekuwa akinyoshewa kidole kwa kashfa mbalimbali, ikiwamo ya ufisadi wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
Aliwahi kudaiwa kuuza kinyemela sehemu yenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe, Kiwira kwa Kampuni ya Tan – Power Resources (TPR).
Kutokana na kashfa ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara, mwaka ….
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.