30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

BODI YATISHIA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma stashahada (Diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/19.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, ilisema mpango huo umesitishwa kama ilivyotangazwa na Serikali.

Mei 10, mwaka huu, HESLB ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Pamoja na mambo mengine mwongozo huo unaeleza bodi hiyo itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa utaratibu wa kuomba mikopo kwa wanafunzi hao ungetolewa baadae.

Taarifa hiyo, ilisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha Sh bilioni 427.5, zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2018/19, zinaelekezwa kwa wanafunzi wenye mikopo hivi sasa na waombaji wapya wenye sifa za kujiunga na kozi za shahada tu ambao ndiyo walengwa wakuu.

“Tunatoa wito kwa wanafuzi wote wenye sifa za kujiunga na masomo ya shahada katika taasisi za elimu ya juu na  wahitaji wa mikopo kuhakikisha wanasoma kwa makini mwongozo wa utoaji mikopo na kuuzingatia,”ilisema taarifa hiyo.

Takwimu za mwaka 2017/18, zinaonyesha karibu maombi 10,027 ya mikopo yaliyowasilishwa ndani ya bodi yalikuwa na upungufu kama vile kutosainiwa na kukosa viambatanisho sahihi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles