28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Miamba yote VPL kukutana Dar

WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

SERIKALI imetenga vituo viwili vitakavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja(FDL) la Pili (SDL)na michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambayo ni Dar Es Salaam na Mwanza.

Ligi hizo zimeruhisiwa kurejea kuanzia Juni Mosi, mwaka huu baada ya kusimamishwa na Serikali kwa zaidi ya miezi miwili ikiwa ni tahadhari ya kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona.

Kutokana na ruhusa hiyo ya michezo kuendelea iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, ametangaza vituo vitakavyotumika kuwa ni Dar es Salaam na Mwanza.

Mwakyembe alisema Dar es Salaam zitachezwa mechi za Ligi Kuu na kombe la shirikisho, viwanja vitakavyotumika ni Taifa, Uhuru na Azam Complex.

Alisema Kituo cha Mwanza zitachezwa mechi za Ligi Daraja la Kwanza na la Pili, timu zitatumia viwanja vya CCM Kirumba na Nyamagana.

Aidha amezihimiza taasisi zinazohusika na  usimamizi ligi hizo zihakikishe ratiba ya michezo hiyo inatolewa mapema ili mashindano hayo yafanyike kwa ufanisi.

“Tunaruhusu Ligi nne kwanza kwa kuanzia, hali ikiendelea vizuri tunafungulia michezo yote, kwa sasa ni Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Kombe la Shirikisho la Azam,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Baada ya kauli ya waziri huyo, MTANZANIA iliwatafuta baadhi ya viongozi na makocha wa  timu za Ligi Kuu kuzungumzia walivyopokea, hasa kucheza  katika kituo kimoja na kuonekana wamelipokea bila tatizo.

Mecky Mexime ni Kocha Mkuu wa timu ya  Kagera Sugar, alisema  hana  hofu anaweza kutumia uwanja wowote atakaopangiwa, kikubwa ni kufanya maandalizi ya kukabiliana na mechi.

“Timu yangu iko tayari  kucheza sehemu yoyote hata tukiambiwa chumbani hakuna tabu muhimu matokeo, kutokana na hili janga  najua viwanja vya Dar es salaam viko salama zaidi kwa wachezaji, naona ni uamuzi mzuri,”alisema Mexime.

Alisema anafahamu wapo watakaopinga  uamuzi huo kutokana dhana iliyojengeka kuwa kutumia viwanja  vya nyumbani kunaleta matokeo mazuri, lakini si kweli.

Naye Mkurugenzi wa Klabu ya Singida United, inayoshika nafasi ya mwisho katika Ligi Kuu, Festo Sanga, alisema maamuzi ya kutumia viwanja vya Dar Es Salaam ni salama na rahisi.

“ Hatuwezi kupingana na Serikali yetu, sisi Singida United tunaona ni sawa kutumia mfumo huyo wa kituo kimoja, hii dhana ya  kwamba matokeo mazuri yanapatikana  viwanja vya  hakuna , huu ni  wakati wa kulindana na janga hili la Corona”alisema Sanga.

Mwingine aliyetoa maoni yake ni Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi, alisema hakuna tatizo kubwa wanalijipanga nalo ni kuhakikisha wanapambana kusalia katika ligi hiyo kwa msimu ujao.

“Kipindi hiki tunapambana na janga la Corona, lazima kufuata yale tunayoelekezwa na wataalamu wetu, naona walichoamua Ligi kuchezwa sehemu moja ni jambo zuri kwa kipindi hiki,” alisema Njashi.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Ndanda FC, Selemani Kachele, alisema wamekubaliana na uamuzi huo, wanasubiri barua naratiba kujua  ni wapi wataweka kambi.

“Hayo maamuzi yameshatoka hakuna budi kuyakubali, hapa tunasubiri taarifa ya mwisho ili kujipanga tutafanyaje mazoezi kwa sababu badi hakuna ratiba ya michezo iliyotoka,” alisema Kachele.

Katibu wa Tanzania Prisons, Ajab Kifukwe, alisema utaratibu utakaotumika utazinyima timu kupata faida ya uwanja wa nyumbani  kwa sababu nyingi zitakuwa kama zinacgeza ugenii.

Alisema kwa sababu barua rasmi kutoka Bodi ya Ligi,  hawajapata wala ratiba, hajafahamu gharama irakuwaje ya kuziweka timu kituo kimoja, kama kila mmoja anajigharamia itakuwa ni changamoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles