31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Chelsea wapanga kuachana na N’Golo Kante

 CHELSEA, ENGLAND 

UONGOZI wa timu ya Chelsea, umedai upo tayari kumruhusu kiungo wao N’Golo Kante kuikosa michezo yote iliyobaki ya msimu huu wa 2019-20 kama ataendelea kuwa na hofu ya kuenea kwa virusi vya corona. 

Alhamisi wiki hii mchezaji huyo alijiunga na wachezaji wenzake katika maandalizi ya mazoezi ya pamoja mara baada ya kufanyiwa vipimo, lakini hakuweza kufanya mazoezi na kuomba kurudi nyumbani kutokana na hofu hiyo ya virusi vya corona. 

Mchezaji huyo raia wa nchini Ufaransa, amekuwa na matatizo ya kiafya siku za hivi karibuni ambapo alianguka mazoezini siku chache kabla ya ligi kusimama kutokana na kusumbuliwa na tatizo la moyo. 

Hata hivyo mchezaji huyo alimpoteza kaka yake kutokana na tatizo hilo la moyo. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Chelsea wamedai wapo tayari kumuacha akapumzika hadi mwisho wa msimu huu kama bado ana hofu na corona hadi pale atakapokuwa sawa.

Kocha wa timu ya Chelsea, Frank Lampard, amedai anaungana na bingwa huyo wa Kombe la Dunia mwaka 2018 kwa kuwa afya ni kitu muhimu kuliko kitu kingine. 

Mchezaji huyo amekuwa na hofu kutokana na taarifa kwamba watu wenye ngozi nyeusi ni rahisi kupata maambukizi hayo ya virusi vya corona. 

 Kante amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Chelsea kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, lakini msimu huu amecheza jumla ya michezo 18 ya Ligi Kuu England na kupachika jumla ya mabao matatu. 

Mbali na mchezaji huyo kubaki nyumbani, lakini amepewa mazoezi maalumu ya kuendelea kujiweka sawa hadi pale atakapokuwa tayari. 

Mchambuzi wa michezo wa kituo cha Sky Sports, Gary Neville, anaamini mbali na Kante, lakini kutakuwa na wachezaji wengine wengi ambao wana hofu kama hiyo huku Ligi ikitarajiwa kurudi mwezi ujao. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles