26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Miaka mitatu baada ya kuondolewa Mugabe, matumaini bado Zimbabwe

HARARE, ZIMBABWE

MIAKA mitatu kamili imetimia tangu kuondolewa madarakani aliyekuwa rais wa Zimbambwe, hayati Robert Mugabe. 

Kiongozi huyo alilazimishwa kujiuzulu Novemba 21, 2017, akihitimisha karibu miongo minne ya utawala wake wa kiimla. 

Kujiuzulu kwake kulifanyika siku kadhaa baada ya vifaru vya kijeshi kupiga doria katika jiji la Harare. 

Mapinduzi dhidi ya Mugabe yalikaribishwa kwa shangwe na maelfu ya watu walimiminika barabarani kusherehekea hatua hiyo. 

Lakini wadadisi wanasema leo hii, miaka mitatu baada ya mrithi wake Emmerson Mnangagwa kuchukua madaraka matumaini makubwa ya mabadiliko yameingia katika hali isiyoeleweka kabisa. 

Ibbo Mandaza, kiongozi wa asasi zinazojihusisha na siasa na uchumi wa upande wa kusini mwa Afrika amesema hakuna kilichobadilika, na mambo yameendelea kuwa mabaya zaidi. 

Amesema viwango vya umasikini na ukandamizaji vimeongezeka zaidi.

Pamoja na hayo, Rais Mnangagwa amekuwa akihangaika kuhakikisha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo vinaondolewa lakini imekuwa bila mafanikio yanayoridhisha.

Amewahi kukiri kwamba vikwazo hivyo vinalemaza ufanisi wa taifa hilo, na kusema vinafaa kuondolewa bila masharti yoyote.

“Tunataka kuondolewa vikwazo vya kiuchumi na kisiasa ambavyo vimelemaza maendeleo ya taifa hili bila masharti yoyote.

“Tunafahamu kwamba kutengwa sio jambo la kujitosheleza, kwani kuna mengi ya kuafikia kupitia umoja na ushirikiano unaofaidi pande zote, ambao unatambua mahitaji ya kipekee ya taifa letu.

“Serikali yetu itaanza upatanisho mpya ili kudhibitisha kwamba tuko miongoni mwa jamii ya kimataifa.” Alisema kiongozi huyo katika kauli ambayo ilionekana kuwapa wengi matumaini ya kubadilisha hali.

Machi 20 mwaka huu ni kama Marekani ilitonesha kidonda baada ya kuwawekea vikwazo viongozi wawili Zimbabwe.

Waziri wa usalama Owen Ncube na balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania Anselem Sanyatwe waliwekewa vikwazo na Marekani kwa kuhusika na mashambulizi dhidi ya wapinzani.

Marekani iliwawekea vikwazo viongozi wawili wa Zimbabwe kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Wizara ya fedha ya Marekani ilielezea kwamba viongozi hao walihusika na mashambulizi dhidi ya waandamanaji nchini humo.

Hatua ilikuja wiki moja tu baada ya Marekani kuongeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.

Taarifa ya wizara ya fedha ya Marekani ilieleza kuwa Waziri wa Usalama wa Zimbabwe, Owen Ncube amewekwa katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Marekani kufutia tuhuma kwamba aliwaamuru maafisa wa usalama wa nchi hiyo kuwavamia na kuwatesa wanachama wa upinzani.

Kwa upande wake, Anselem Sanyatwe, Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, yeye alituhumiwa kuongoza mashambulizi ya maofisa wa usalama dhidi ya wapinzani baada ya uchaguzi wa mwaka 2018. 

Wakati huo Sanyantwe alikuwa akiongoza kitengo cha ulinzi wa rais kwenye jeshi la taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles