30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Miaka 7 kifo cha Michael Jackson… Haya ndiyo maisha ya watoto wake  

michael-jackson-kids-paris-prince-blanket-2012Na FARAJA MASINDE

NI miaka saba sasa tangu kuondoka duniani kwa mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson ambaye aliacha watoto watatu ambao ni Paris, Prince na Blanket Jackson.

Mfalme huyo wa Pop alikuwa akijaribu kuwaweka karibu watoto wake hao enzi za uhai wake na hivyo kujikuta akipamba makava ya majarida mbalimbali ya habari akiwa na familia yake hiyo.

Hata hivyo mara baada ya kifo chake, familia yake hiyo bado imeendelea kusonga mbele katika maisha yao ya kutokupenda kuonekana mara kwa mara mitaani licha ya kwamba wamekuwa wakubwa.

Hata hivyo watoto hao wapo ambao wameamua kufuata nyayo za baba yao kwa maana ya kuingia kwenye tasnia ya muziki huku wengine wakiwa na shughuli nyingine ambazo zimekuwa zikiwaingizia vipato.

Je, unajua wanachofanya watoto wake? Swaggaz limechimba na linakupa madini hapa chini.

 

Michael Joseph Jackson Jr.

Huyu ni mtoto wa kwanza wa marehemu Michael Jackson mwenye umri wa miaka 19. Jackson Jr ambaye ni maarufu kwa jina la Prince Michael, alianza kufanya kazi kwenye kituo cha televisheni kwenye kipindi cha burudani kinachofahamika kama ‘Entertainment Weekly” na kile cha “90210”.

Kufuatia kazi yake hiyo kwenye Tv, Prince ameanza kuonekana mbele ya uma tofauti na awali ambapo ilikuwa ngumu kuwaona watoto hao wa Michael wakiwa hadharani.

Mwaka jana, Prince alihitimu masomo yake ya elimu ya juu ambapo kwa sasa licha ya kuwa na kipindi kwenye runinga pia anasoma katika Chuo Kikuu cha Loyola Marymount, ambapo pia amekuwa ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuwasiliana na watu waoamfuata kwenye mtandao huo.

 

Paris-Michael Katherine Jackson

Paris (18) ambaye ni mtoto wa pili wa mfalme huyo, tofauti na watoto wote wa Michael, yeye amekuwa akionekana zaidi hadharani.

Kufuatia kifo cha baba yake, Paris na kaka yake walifanya onyesho maalumu la kumuenzi baba yao ambalo lilipewa jina la ‘Various Michael Jackson’. Mara nyingi, Paris amekuwa akionekana mitaani akiwa amevaa  tisheti yenye sura ya baba yake.

“Baba yetu alikuwa baba bora kuliko mababa wengine duniani, napenda tu niseme kuwa nampenda sana baba yangu licha ya kwamba hayupo nasi tena hii leo,”anasema Paris.

Licha ya kwamba mambo yalikuwa yakimwendea vyema, mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 15 alijaribu kujiua. Hata hivyo mpango wake huo ulikwama na hajawahi kujaribu tena kitendo hicho tangu kipindi hicho na kwa sasa amekuwa akijihusisha zaidi na kushughulikia uhalifu wa kimtandao.

Mapema mwezi huu, Paris alijirekodi video na kuituma kwenye mtandao wa YouTube ambapo katika video hiyo alisikika akisema kuwa anajihisi kama mtu anayechukiwa na dunia kwa sasa na kuongeza kuwa amekuwa akijaribu kupambana mwenyewe kwa kutumia mitandao na vitu vyote vinavyomchukiza na kwamba amekuwa akijaribu kufanya vitu vingi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anakaa mbali na maadui zake lakini imekuwa ngumu.

 

Blanket Michael Jackson II          

Blanket (14) ambaye huyu amekuwa akitajwa kama mtoto anayetaka kufuata nyayo za baba yake kutokana na kuwa maarufu pamoja na kupenda kujihusisha na muziki. Ili kudhihirisha hilo, tayari amebadili jina lake na kujiita ‘Big Jackson’.

Anasema ndoto yake hiyo ya kuja kuwa mwanamuziki alikuwa nayo tangu akiwa na hayati baba yake.

 

Michael Jackson kwa ufupi

Marehemu Michael Jackson alizaliwa Agosti 29, 1958 kwenye eneo la Gary, Indiana na kufariki dunia Juni 25, 2009 huko Los Angeles, California. Mbali ya kuwa mwanamuziki, pia alikuwa mtayarishaji, mtunzi wa nyimbo, mwimbaji na dansa.

Mauzo ya albamu yake ya Thriller aliyoitoa mwaka 1982 yameendelea kuweka rekodi mpaka hivi leo duniani kote.

Familia yake kwa sasa inaishi mjini Califonia,  Marekani na mama yao ambaye Deborah Jeanne “Debbie” ambaye kitaaluma ni nesi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles