27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Miaka 60 ya Uhuru| Serikali mbioni kukamilisha utekelezaji mfumo wa mafao

*Yajivunia Tume Huru ya Uchaguzi

*Sekta ya hifadhi ya jamii yazidi kuimarika

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

OFISI ya Waziri Mkuu imesema inakamilisha utekelezaji maelekezo ya Serikali juu ya kuimarisha Mfumo wa Mafao ya Watumishi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii huku ikiibainisha kuwa ndani ya kipindi cha Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara imepata mafanikio kadhaa.

Hayo yamebainishwa leo, Jumanne Novemba 23, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 60 ya uhuru na kuongeza kuwa anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuangalia utaratibu wa kulipa madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

“Kwa sasa Ofisi ya Waziri Mkuu inakamilisha utekelezaji maelekezo ya Serikali ya kuimarisha Mfumo wa Mafao ya watumishi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

“Naishukuru Serikali ya Mama Samia inaendelea kuangalia madeni haya yote na kuona utaratibu wa kulipa na inafanya utaratibu wa kulipa Shilingi Trilioni  4.6. Tunaamini kwa mwenendo huu kwa Commitment ya serikali  tunapoenda madeni yataisha  na utatengenezwa mfumo bora,”amesema Mhagama.

MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA PSSSF KIGANJANI

Waziri Mhagama amesema kuwa mfumo wa Kielekroniki wa PSSSF Kiganjani una maeneo mawili, eneo la Wanachama na jingine ni la waajiriwa ambapo amedai unatoa fursa kwa mwanachama ya kupata taarifa ya mwajiri kuhusu mawasilisho ya michango ya wanachama, usajili na madeni ya michango yake ambayo haijalipwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Pia unarahisisha upatikanaji wa taarifa za michango ya wanachama sambamba na ufuatiliaji wa malipo ya Pensheni ya kila mwezi kwa mwanachama.

Aidha, amesema tangu Tanzania ipate uhuru, sekta ya hifadhi ya jamii imepitia mabadiliko chanya yaliyolenga kuboresha huduma za hifadhi za jamii kwa Watanzania.

Amesema Mwaka 1962, serikali ilipanua wigo wa watumishi wanaohudumiwa na  mfumo wa pensheni kwa kuwajumuisha Waalimu wazalendo kwani kabla ya hapo mfumo ulikuwa unahudumia watumishi wa Serikali Kuu pekee.

Ameongeza kuwa mwaka 1964 ulianzishwa Mfuko wa Akiba kwa watumishi kwa Sekta Binafsi (NPF) baadaye mwaka 1998 ulianzishwa Mfuko wa NSSF ambao unahudumia watumishi wa Sekta Binafsi (kwa sasa).

Hata hivyo, mifuko ya GEPF (1942), LAPF (1944) iliyokuwa imeanzishwa kabla ya Uhuru ambayo ilihusisha wafanyakazi wa serikali kuu waliokuwa wa mikataba (Non Pensionable) na wafanyakazi wa serikali za mitaa.

Waziri huyo amesema mwaka 2010, 2014 na 2018 serikali iIifanya mabadiliko makubwa ya kuboresha  sekta ya hifadhi ya jamiiambapo ilianzisha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Pia, mwaka 2014 serikali ilifanya mabadiiko ya sheria ya SSRA ili kuwianisha mafao kwa watumishi wanaostaafu katika sekta ya umma na binafsi.

“Mwaka 2008, serikali ilitunga sheria mpya na kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanya Kazi (WCF) ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2015 ili kuondokana na sheria ya fidia kwa wafanyakazi ya mwaka 1957 na mapitio yake ya mwaka 2002 ambayo haikuwa inatenda haki katika kuoanisha viwango vya malipo ya fidia kwa ulemavu na madhara yatokanayo na kazi.

“Mwaka 2018 serikali iliunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii minne ya GEPF, LAPF, PSPF na PPF kuwa mfuko mmoja wa PSSSF wa watumishi wa Umma,” amesema Waziri Mhagama.

VYAMA VINGI

Waziri huyo amesema Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi vya Siasa ulikuwapo kabla na baada ya uhuru.

“Kati ya mwaka 1965 mpaka 1992 tulikuwa na mfumo wa chama kimoja. Mwaka 1992 nchi yetu ilirejesha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa ili kupanua wigo wa demokrasia,”amesema Waziri Mhagama.

Amesema mwaka 1992, sheria ya vyama vya siasa na. 5 ilitungwa na kuanzishwa kwa fisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini.

“Vyama vya siasa vilianza kusajiliwa tena mwaka 1992 ambapo katika Uchaguzi Mkuu wa vyama vingi vya Siasa mwaka 1995 vyama vya Siasa 13 vyenye usajili kamili viliweka wagombea.

“Toka mwaka 1992 mpaka sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imekwisha toa vyeti vya usajili wa muda kwa vyama vya Siasa 81 na imetoa vyeti vya usajili kamili kwa vyama vya Siasa 25 na kufuta usajili wa vyama vya Siasa vyenye usajili kamili 6 ambavyo vilikiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

“Toka mwaka 1992 mpaka sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwisha toa vyeti vya usajili wa muda kwa vyama vya Siasa 81 na imetoa vyeti vya usajili kamili kwa vyama vya Siasa 25 na kufuta usajili wa vyama vya Siasa vyenye usajili kamili 6 ambavyo vilikiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa,”amesema.

Amesema, hivi sasa kuna  vyama vya siasa vyenye usajili kamili 19 na Chama kimoja cha siasa chenye usajili wa muda.

Aidha, Sheria ya vyama vya Siasa imekuwa ikiboreshwa mara kwa mara ili kuendana na mahitaji ya wakati husika na kuiwezesha kukabili changamoto zilizopo na zitakazojitokeza. 

TUME HURU YA UCHAGUZI

Waziri Mhagama amesema mafanikio ambayo imeyapata ndani ya miaka 60 ya uhuru ni kuwa na  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni huru na inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na wala serikali haiingilii majukumu yake.

Waziri huyo amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa  Januari, 14 mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(i) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.

Aidha, Ibara ya 74 (7) na (11) inaeleza kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Huru na katika utekelezaji wa majukumu yake haipokei amri au maelekezo kutoka kwa mtu au Taasisi yoyote.

Amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuendesha, kusimamia na kuratibu Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani chini ya Mfumo wa Siasa wa Vyama Vingi.

Amesema Mmjukumu mengine ya Tume ni pamoja na Kusimamia na kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara; Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Majimbo ya Uchaguzi wa Wabunge na Kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchini kote.

Amesema mpaka sasa Tume ya Uchaguzi imefanikiwa kusimamia Chaguzi Kuu 6 za mwaka 1995, 2000, 2005, 2010,2015, 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles