29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 7, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Miaka 22 Miriam Odemba aendelea kupeta

BRIGHTER MASAKI

HESHIMA kwenye tasnia ya mitindo inaletwa na wanamitindo wenyewe. Miriam Odemba ni miongoni mwa ‘icon’ za mitindo Bongo ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga la Kimataifa.

Mrembo huyo mwenye makazi yake  nchini Ufaransa hivi sasa amerejea nyumba kufanya shughuli za kijamii kupitia taasisi yake ya Miriam Odemba Foundation.

Mapema juzi mrembo huyo daraja la kwanza alitua katika shule ya Kiwambo huko Mkuranga, Pwani kuzindua kisima cha maji na akapiga mastori kibao na Swaggaz kama ifuatavyo.

Swaggaz: Umeitumikia tasnia ya mitindo kwa miaka 22 sasa, je unajitofautisha vipi na warembo wengine?

Odemba: Nyinyi wenyewe mnaona jinsi  ninavyofanya kazi zangu, ninakuwa karibu na wanavijiji, nimekuja kufanya kazi za kijamii na ninataka nibadilishe umasikini Tanzania na kuwasaidia Watanzania wenzangu.

Katika hiyo miaka 22 ya Kkuwepo kwenye mitindo nimefanikiwa sana namshukuru Mungu pia nimeokoka na sasa nataka nifanye kazi ambayo itaweza kuwasaidia wadogo zangu waweze kufuata nyayo zangu.

Siyo mtu akupe kama mimi nilivyopewa na marehemu Amina Mongi, Maria Sarungi  au Ruge Mutahaba. Mimi sikupata elimu sana na sasa hivi nataka niwezehse kutoa elimu kubwa kwa wanafunzi wapate elimu zaidi na wao wataweza kusaidia mama zao na familia zao, hakuna modo yeyote anayefanya kazi kama hizi za kutembelea mashule na kuangalia matatizo yao.

Miriam Odemba

Swaggaz: Kukosa elimu ya darasani  kumefanya ukose vitu gani kwenye mitindo?

Odemba: Sijapata elimu kubwa ya darasani lakini nimepata elimu ya maisha, nimefunzwa na ulimwengu na nimetembea duniani nchi nyingi sana ndiyo maana sasa hivi nasaidia kina mama na watoto kwasababu wao ndiyo nyumba ya Taifa.

Swaggaz: Changamoto gani uliipitia katika safari yako ya mitindo ambayo hutaki wadogo zako wazipitie?

Odemba: Kwakweli mimi ninachoona ni elimu. Elimu ni kitu kikubwa sana, elimu ndiyo pochi yako.

Swaggaz: Unadhani kwanini warembo wengi huwa wanaanguka pindi wanapopata umaarufu?

Odemba: Siwezi kuongelea warembo wengine labla hali wanayopitia hapa Tanzania kwasababu mimi tokea nilivyoanza mitindo nilikuwa mdogo, nimetoka Tanzania nina miaka 16 nikaenda nchi za nje nadhani mtazamo wangu siko kama Watanzania lakini nimetoka kwenye familia  ya kimasikini na nilipata uchungu sana nikasema malengo yangu lazima niyatimize nikipata tu pesa.

Ningependa kuwapa ushauri warembo wa Tanzania waweze kuangalia vitu ninavyofanya na kama wanataka kushirikiana na mimi mlango upo wazi nitawapa siri kubwa katika kusaidia jamii maana peke yangu sitaweza kutokomeza umasikini lakini tukishirikiana wote warembo, wanamuziki tutaweza pia na serikali imekuwa ikitusaidia sana maana ukienda kwa viongozi kama Dc Jokate Mwengelo wanatusaidia.

Odemba akiwana watoto kwenye shughuli za kijamii.

Swaggaz: Kwanini umekuwa ukiweka maisha yako ‘private’ tofauti na mastaa wengine?

Odemba: Maisha yangu yapo ‘private’ sababu nimeokoka nampenda Mungu sana nadhani pia nasoma sana vitabu na Biblia na sifanyi vitu vya ajabu sababu nimemuweka Mungu kuwa namba moja.

Swaggaz: Umekuwa na urafiki na wanamuziki mbalimbali na sasa hivi kuna mvutano wa kutumbuiza katika matamasha ya Wasafi Festival, Fiesta, Mziki Mnene nk, je unawapa ushauri gani wasanii?

Odemba: Kama ulivyosema nina naheshimika sana Tanzania, mimi nina ile kitu ambayo nimejiwekea, sipendi kuvunja heshima yangu ndiyo maana ukiona wasanii wakubwa wote naongea nao awe Alikiba, awe Harmonize, awe Diamond Platnumz na jana (Jumatano) nilipata tuzo ya heshima kutoka kwa Diamond sababu ameona kazi yangu kwa jamii. Mimi nipo timu zote, wasanii wote nawapa sapoti na wao waje tu kunipa sapoti kwenye shughuli zangu za kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles