25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MIAKA 22 BILA TUPAC, MATENDO YAKE MEMA YAENZIWE


NA CHRISTOPHER MSEKENA

Wiki hii sekta ya burudani iliadhimisha miaka 22 ya kifo cha Tupac Shakur (2 PAC), miongoni mwa wasanii wachache walioacha alama isiyofutika katika muziki wa hip hop duniani.

Tupac alifariki dunia Septemba 13 mwaka 1996 katika Hospitali ya University Medical Center huko Las Vegas Nevada nchini Marekani baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Toka mwana hip hop huyo na msanii wa filamu apoteze maisha, dunia imekuwa ikiadhimisha kumbukumbu yake kila mwaka huku makundi mbalimbali yaliyokuwa yanamkubali Tupac yakifanya mambo ya kumuenzi.

Licha ya kuishi miaka 25 tu katika dunia kabla ya kifo chake kazi ya Tupac imeendelea kuleta mchango chanya utadhani aliishi maisha marefu, ameendelea kuishi kwenye nafsi za watu hususani vijana.

Utakuwa shahidi wa hili kwa kuwa si jambo la ajabu kukutana na vijana wakiwa wamejiweka katika mwonekano aliokuwa nao Tupac. Vijana wananyoa urapa na kujifunga vitambaa ‘bandana’ kichwani.

Tupac amewaambukiza vijana wengi tabia ya kuwa wakweli na wawazi katika kutoa mawazo yao bila kuogopa, kuzungumza kile wanachokiamini hata kama kinaweza kuhatarisha maisha yao.

Hali kadhalika wasanii wengi duniani wakiwamo hapa Tanzania, wamekuwa wakipita kwenye utunzi unaofanana na ule ambao Tupac alikuwa anautumia katika ngoma zake ambazo zinaishi mpaka leo.

Tupac alifanikiwa kwenye sanaa kutokana na maudhui ya kazi zake kuwa za kipekee jambo ambalo lilimtofautisha na wasanii wengine wa rika lake kiasi cha kazi hizo za muziki na filamu kuingiza fedha mpaka leo.

Atakumbukwa kuwa ndiye msanii wa hip hop aliyetambulisha mtindo wa wasanii wa muziki huo kuwekeza fedha nyingi katika video zake ili kupata ubora kabla ya wasanii wengine kufuata nyayo zake.

Ndiyo maana mabadiliko makubwa yamekuwa yakifanyika kadiri muda unavyokwenda kwa wasanii wa hip hop kuwekeza katika ngoma zao baada ya Tupac kuthubutu kufanya kitu cha tofauti na ilivyozoeleka.

Tukirudi hapa Tanzania, tunaona wasanii wetu wanajitahidi kuthubutu kufanya mambo ambayo hayakuwapo hapo nyuma jambo ambao ni jema na lina akisi kuenziwa kwa Tupac ikiwa ni maadhimisho ya miaka 22 ya kifo chake.

NUKUU

“Nikiwa hospitalini ICU aliletwa jamaa aliyepigwa risasi tisa mwilini, madaktari walifanikiwa kuokoa maisha yake, akapona hapo nikajifunza kuwa kuugua siyo kufa,”

Ommy Dimpoz.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles