28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MEYA KINONDONI APELEKA MABILIONI KWA VIJANA

NA MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

KATIKA kusaka njia sahihi za kupambana na changamoto ya uhaba wa ajira nchini, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta, ameamua kuelekeza kiasi cha Sh bilioni 4.5 kwa vijana.

Kiasi hicho cha fedha, mbali ya kuwanufaisha vijana, pia kitakuwa ni msaada mkubwa kwa wanawake wa Halmashauri hiyo, ambao kwa pamoja watapatiwa mikopo itakayowasaidia kuanzisha na kuendeleza biashara zao.

Kwa mujibu wa Meya Sitta, kiasi hicho cha fedha kimepangwa kutumika ndani ya miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2017/18.

Ili kufanikisha nia hiyo ya kuwasaidia vijana na akina mama, katika mwaka huu wa fedha kiasi cha Sh bilioni 1.5 zimetengwa, ambapo fedha hizo ni sawa na asilimia 10 ya mapato yatokanayo na makusanyo ya ndani kwa mwaka, ikiwa ni utekelezaji wa sera inayozitaka Halmashauri na Manispaa zote nchini kutenga mifuko maalumu.

Neema hiyo kwa wanawake na vijana imetangazwa juzi na Meya Sitta, alipokuwa katika ziara ya kikazi iliyomkutanisha na wakazi wa Kawe, jijini Dar es Salaam, ambako pamoja na mambo mengine, alisikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo, Meya Sitta alitoa wito kwa makundi yenye sifa kuchangamkia fursa ya fedha hizo na kuzifanyia kazi ili kujiondoa kwenye tatizo la kukosa ajira, lakini pia kujiongezea kipato.

Aliwaambia wakazi hao kuwa, halmashauri hiyo imeanza kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kwa ajili ya kujenga stendi ya kisasa ya mabasi ya daladala Kawe na maeneo ya wafanyabiashara wadogo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles