26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MEYA DAR KUPASUA JIPU LA UDA LEO

1.Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, leo anatarajia kuibua madudu ya mkataba wa ufisadi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) na Kampuni ya Simon Group Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara, Robert Kisena.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Meya Mwita alisema  atazungumzia  suala hilo   baada ya kuupitia upya mkataba huo na kubaini kuwapo ukiukwaji wa sheria wakati wa makubaliano ya mkataba.

“Kesho (leo), nitakutana na waandishi wa habari pale Karimjee Hall kuwaeleza ukweli wa mkataba wa Uda, tumefikia pazuri tunataka umma ujue,” alisema.

Alipoulizwa ni nini hasa amepanga kukizungumzia, Meya Mwita alisema: “Usitake nizungumze kila kitu hapa, nitumie mwandishi Jumatatu saa tatu asubuhi pale Karimjee Hall… sawa ndugu yangu”.

Alisema   Halmashauri ya Jiji  iliitisha vikao vya baraza la madiwani pamoja na watendaji   kujadili suala hilo na kukubaliana kwa pamoja kulizungumza hadharani  wananchi waweze kulijua.

“Baada ya kuingia madarakani tumeupitia upya mkataba wa Uda   tuweze kuangalia uhalali wake pamoja na udhaifu, hali iliyofanya kubaini kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa  sheria uliofanywa na waliokuwa viongozi wa jiji wakati wa kuingia mkataba huu na Kampuni ya Simon Group Limited,” alisema Mwita.

Alisema uongozi wake hauwezi kuvumilia suala hilo kwa sababu linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Mwita alisema ni  lazima jambo hilo lizungumzwe hadharani wananchi waweze kujua madudu yaliyofanyika.

“Tumefanya vikao mbalimbali kwa ajili ya kujadili mkataba huu lakini hapana.

“Hatuwezi kukaa kimya lazima tulizungumze suala hili hadharani   kila mmoja aweze kupima utendaji kazi wa viongozi waliopita,” alisema.

Awali, Uda ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja na  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu kupitia Hazina, wakiwa na   hisa za Sh milioni 15 kila hisa moja ikiwa na thamani ya Sh 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles