24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Bukoba atoa siku tatu kwa mkuu wa shule kukamilisha ujenzi wa madarasa

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Godson Gypson pamoja na wenyeviti wa Kamati za kudumu wa Halmashari hiyo ametoa siku tatu kwa Mkuu wa shule ya Sekondari Buhembe, Constantine Nyawawa kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasashuleni hapo huku akimtaka Ofisa elimu sekondari, Frances Nshaija kufuatilia ili kubaini kama kuna uzembe umefanyika katika ujenzi na kuchukua hatua.

Gypson ametoa maagizo hayo jana Desemba 11, 2021 katika ziara na madiwani wenzake kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 30 katika kata 14 za Manispaa ya Bukoba vinavyojengwa kwa fedha za uvico-19 zilizotolewa na Serikali Sh milioni 600.

Meya wa Manispaa ya Bukoba, Godson Gypson, akishiliki ujenzi katika shule ya Sekondari Kibeta.

Meya Gypson akiwa na madiwani baada ya kufika kata ya Buhembe hakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na hivyo akatoa siku tatu kwa mkuu wa shule hiyo kuhakikisha anasimamia ujenzi pasipo kupoteza Muda.

“Nitumie Fursa hii kuwaomba wakuu wa shule na wasimamizi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kuhakikisha hawaruhusu jambo lolote linaloweza kutukwamisha ili twenda na Kasi tuliyoipokewa kutoka juu,” amesema Meya wa Manispaa ya Bukoba.

Ofisa elimu sekondari Manispaa ya Bukoba, France Nshaija amesema kuwa, shule ya sekondari Buhembe bado iko kiwango cha chini cha ujenzi kati ya 50 hadi 60 asilimia huku sekondari nyingine zikiwa hatua ya kukamilisha kati ya 85 hadi 90 asilimia.

Amesema hata hapo ujenzi ulipofikia idara ya yake imekuwa akifanya ukaguzi wa mara kwa mara na ataendelelea kufanya hivyo ili ujenzi ukamilike kwa wakati katika shule hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Constantine Nyawawa amesema kuwa, kuchelewa kwa ujenzi kumesababishwa na kubadilisha mzabuni ambapo awali waliagiza vifaa kama misumali, na mabati mzabuni akashindwa kuvileta kwa wakati ikabidi wabadilishe watafute mzabuni mwingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles