Elizabeth Kilindi, Iringa
Kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii mkoani Iringa, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada, ametoa wito kwa watalii kujitokeza kwa wingi ili kujionea maajabu.
Ngwada ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari wanawake kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini walipomtembelea ofisini kwake ambapo amesema utalii unachangia kukuza pato la mkoa huo.
‘’Hadi sasa tayari utalii unachangia kwa kiasi kikubwa pato la mkoa wetu kwa sababu wapo watalii wengi ambao wanakuja, wanataka kujifunza kuhusu chifu Mkwawa,kwenda Ruaha pamoja na makumbusho ambayo yanaelezea kuhusua mkoa wa Iringa’’amesema Ngwada.
Meya Ngwanda amesema mkoa wa Iringa ni mahali pazuri kwa ajili ya kuwekeza kwa sababu ni jirani na makao makuu ya nchi.
‘’Bado tunahitaji watu wengi waje wawekeze Iringa,Halmashauri yetu ndio sehemu sahihi kwa sababu kuna maeneo ya kuwekeza hoteli,majengo makubwa kwa sababu mtu anaposhindwa kufanya jambo katika Mkoa wa Dodoma,sehemu ya karibu ni Iringa.