29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mesut Ozil alimkataa Unai Emery

LONDON, ENGLAND

KIUNGO wa Arsenal, Mesut Ozil, ameripotiwa kuwa, alimkataa kocha wa timu hiyo Unai Emery kwa kumwambia hafai kuwa kocha.

Kwa mujibu wa gazeti maarufu nchini Uturuki, Fanatik, mchezaji huyo aliitoa kauli hiyo baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa fainali wa Kombe la Europa dhidi ya Chelsea wiki moja iliopita.

Ozil alitolewa katika dakika ya 78 na nafasi yake kuchukuliwa na Joe Willock, hivyo Ozil alionekana kuna maneno anayaongea wakati anatoka nje, hivyo gazeti hilo lilitoa tafsiri ya maneno hayo kwamba alisema ‘Naapa kwamba wewe sio kocha.’ Hata hivyo mbali na kufanyiwa mabadiliko, lakini timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 4-1.

Ozil alionekana kutoridhishwa na kitendo cha kufanyiwa mabadiliko, baadhi za picha zilimuonesha akiwa na uzuni wakati yupo nje ya uwanja huku mchezo huo ukiendelea.

Msimu huu Ozil hakuwa kwenye kiwango kizuri cha kuweza kuisaidia Arsenal kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali, hivyo kulikuwa na taarifa za uongozi wa timu hiyo kutaka kuvunja mkataba wake.

Kwa sasa mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2021. Huku akidaiwa kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wanalipwa kiasi kikubwa cha fedha, pauni 350,000.

Hata hivyo, katika baadhi ya michezo Ozil amekuwa akikaa benchi bila ya kujali kiasi hicho cha fedha anacholipwa, hivyo kupelelea mjadala wa kutaka kuachana na mchezaji huyo ili kuweza kupunguza kiasi kikubwa cha mashara ambacho kinatumika bila ya faida.

Katika michezo 35 aliyocheza Ozil msimu huu kwenye michuano mbalimbali amefanikiwa kupachika jumla ya mabao sita huku akipiga pasi tatu za mwisho ikiwa ni tofauti na wengi walivyozoea kumuona mchezaji huyo akiwa kwenye kiwango chake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles