25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Merson aponda usajili Van de Beek Man United

MANCHESTER , ENGLAND

MCHAMBUZI wa soka nchini Uingereza, Paul Merson ameponda uamuzi wa Manchester United kumsajili kiungo wa  Ajax, Donny van de Beek, akimtaja mchezaji huyo mpya wa United kama ‘usajili wa  hofu’.

Kiungo huyo mwenye umri  wa miaka 23 alitua  Old Trafford kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 40 dili lililokamilika wiki iliyopita ukiwa ni usajili wa kwanza wa  Ole Gunnar Solskjaer katika dirisha hili la usajili wa majira ya joto.

Van de Beek  anajiandaa kuungana na mastaa wengine wa United kama  Bruno Fernandes na Paul Pogba ambao ni moyo wa kikosi cha Solskjaer,lakini mchambuzi wa  Sky Sports ,Merson anaamini Mholanzi huyo amesajiliwa ili kupunguza hasira za mashabiki wa timu hiyo kuhusu usajili.

Merson aliliambia  Daily Star: ‘Donny van de Beek amaonekana kama amenunuliwa na  Manchester United kwa hofu, sijui.

“Wametumia Euro milioni 40 kuimarisha eneo ambalo ni imara na vipi atacheza na  Pogba na  Fernandes?

“Una mmoja anayeweza kucheza kama kiungo mkabaji , usajili huio unaoneka hivyo, ooh  bado hatujamnunua mtu yeyote, wacha twende tukanunue mtu, tunaweza kupata nani?”

Kabla ya kumnasa Van de Beek, Manchester United ilikuwa imechanganyikiwa baada ya kushindwa kumsajili winga Jadon Sancho  kutoka Borussia Dortmund.

Nyota huyo wa kimataifa wa England alikuwa tayari kujiunga na United, lakini klabu hiyo ilipewa muda wa kukamilisha dili hilo kabla ya Agosti 10 kwa kutoa dau la Euro milioni 108 .

Solskjaer bado anataka kurudi kwa  Sancho kuanzia sasa hadi mwisho wa dirsha hili la usajili Oktoba  5, hata hivyo United inahusishwa kumsajili beki wa kati wa RB Leipzig, Dayot Upamecano.

Van de Beek ametua  Old Trafford baada ya kufanya vizuri na timu yake ya utotoni ya Ajax, kinda huyo mwenye umri wa miaka 23 aliichezea timu hiyo michezo 175 na kufunga mabao 41.

Alikuwa sehemu ya kikosi cha Ajax kilichotinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 na alifunga bao katika kila mchezo wa  mtoano kabla ya kushindwa kwa kwa Tottenham Hotspur.

Kombe AFCON lapotea kimiujiza Misri 

CAIRO, MISRI

MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri, (EFA), Ahmed Shobir amesema kombe la Mataifa Afrika ( AFCON)  limepotea katika makao makuu ya Shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo, Misri.

Taji hilo la AFCON lilikuwa limehifadhiwa Misri baada ya timu  hiyo kushinda kwa mara tatu mfululizo tangu mwaka 2006 hadi 2010.

Watendaji wa Shirikisho hilo wamedai ya kuwa kombe hilo lilikuwa limehifadhiwa kwa nahodha wa timu ya taifa Misri, Ahmed Hassan, ambaye naye amekanusha hilo na kusema alikaa nalo kwa siku moja baada ya kushinda na alilikabidhi tangu mwaka 2011.

Baada yakuwa mabingwa mara tatu mfululizo , Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliwapatia mfano ( Replica) wa kombe halisi la CAF ili wakae nalo moja kwa moja . 

Kombe halisi walipewa muda mchache tu wakuwa nalo kabla ya CAF kulichukua na kulitunza bank . cha ajabu liliibiwa kabla ya kuihifadhiwa na lawama kutupiwa huyo nahodha ambaye kakana .

Baada ya viongozi wa CAF kusema kombe limeibiwa nyumbani kwa nahodha wa timu ya taifa ya Misri Ahmed Hassan, nahodha huyo amekana tuhuma hizo akisema kombe hilo lilikaa nyumbani kwake kwa siku moja tu na aliwakabidhi CAF tangu 2011. 


Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kombe hilo liliibiwa zaidi ya miaka tisa iliyopita na CAF wameanza kuchunguza kwa tukio hilo kina wakishirikiana na vyombo vya dola kumjua mwizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles