28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Membe: Nikiwa rais wasanii wataenda kujifunza nje

Bernard-MembeJENNIFER ULLEMBO NA MWALI IBRAHIM
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha anasimamia haki za wasanii ipasavyo.
Membe alitoa kauli hiyo mkoani Lindi wakati akitangaza nia ya kuwania urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
“Nitahakikisha naweka mipango imara katika kusimamia kazi za wasanii wote kunufaika na hakimiliki zao,” alisema.
Pia alisema atahakikisha wasanii wanakwenda kujifunza nje ya nchi masuala ya sanaa ili sekta hiyo ipate mabadiliko ya kimaendeleo kwa wasanii na Serikali kwa ujumla.
“Nikichaguliwa kuwa rais, nimejiwekea mikakati mingi kuhakikisha sekta ya sanaa inapiga hatua kutoka hapa tulipo sasa,” alisema Membe.
Katika mkutano huo, waliohudhuria ni baadhi ya wasanii akiwemo mchekeshaji, Adam Melele ‘Swebe’, Hemed Malyaga ‘Mkwere Orijino’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles