23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Meli ya mizigo yazama Bahari ya Hindi

Meli ya mizigo Mv. Happy
Meli ya mizigo Mv. Happy

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MELI ya Mizigo ya Mv. Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda  Zanzibar  imezama katika Bahari ya Hindi   ikiwa imebeba mbao zaidi ya 1090 na magunia 450 ya viazi mviringo.

Hata hivyo,  mabaharia 12 ambao ni wafanyakazi katika meli ya mizigo  ya hiuo wamesalimika kufa maji  kwa vile meli hiyo  haikuzama yote  katika eneo la Kizingo  kisiwani Zanzibar.

Tukio hilo lilitokea jana alfajiri kisiwani Unguja.

Mkuu wa Operesheni baharini, Msilimiwa Idd,  alisema tukio hilo lilitokea saa 8.00 usiku baada ya meli hiyo kuyumba kutokana na dhoroba kali ya upepo.

Alisema ilipotimu saa saa 9.00usiku nahodha wa meli hiyo  alipoona hali imezidi kuwa mbaya akaelekea katika Kisiwa Mchanga  ambako alijikuta akikwama kwa vile upande mmoja wa meli ulikuwa unapitisha maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles