24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Meena: Waandishi wa habari ni jicho la jamii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema, waandishi wa habari wana wigo mpana wa kufikisha taarifa zao na kuifanya jamii ichukue hatua au ishinikize hatua zichukuliwe kulingana na kile walichokisoma, kukisikia au kukiona.

Meena ametoa kauli hiyo Oktoba 22, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia umuhimu wa wanahabari kuchochea maendeleo, uzalishaji mali na mabadiliko ya sheria kwenye warsha ya kuwajengea uwezo wahariri kuandika na kupitia habari za uchechemuzi wa Mabadiliko ya Sheria ya Habari.

“Leo hii mitandao ya kijamii na katuni zimekuwa zikitumika kufikisha ujumbe kwa jamii na kuleta mabadiliko makubwa, cha msingi ni lazima sheria ziweke misingi imara ya Watanzania kuwa na uhuru wa kujieleza, kupata habari na kusambaza,” amesema Meena.

Upande wake, Jabir Idrisa, Mhariri wa Gazeti la MwanaHalisi amesema, jamii inapaswa iendelee kupigia kelele kwa kushirikiana na vyombo vya habari juu ya marekebisho ya sheria zinazokwaza uhuru wa habari.

“Juzi tu kuna mtu kule Simiyu amefungwa miaka 7 na faini ya Sh milioni 15 kwasababu ya kumtukana kiongozi, sheria ya makosa ya mtandao tunayoilalamikia ndiyo imetumika, tuendelee kupigania marekebisho ya sheria zinazominya haki za binadamu,” amesema Idrisa.

Naye, Tumaini Mbibo, amesema watu wanaweza kudhani sheria ni mbaya lakini kumbe hawazijui hivyo jambo la msingi ni kuwawezesha wazijue ili wasizivunje na kuingilia haki za watu wengine

“Hatuwezi kudai mabadiliko ya sheria kama hatuzijui, tufanye uzengezi wa mabadiliko ya sheria tunazozilalamikia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili tupate matokeo chanya,” amesema Mbibo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles