MCHUMBA wa rapa Nicki Minaj, Meek Mill amefanikiwa kuchukua tuzo ya albamu bora na kuwabwaga wakali wa muziki huo, Drake na Kendric Lamar kwenye 2016 Billboard Music Awards.
Msanii huyo ameng’aa kutokana na ubora wa albamu yake ya ‘Dreams Worth More Than Money’ ambapo alikuwa anashindanishwa na albamu ya Kendric Lamar ya ‘To Pimp a Butterfly’ na Drake ‘If You’re Reading This It’s Too Late’ pamoja na Future albamu ya What a Time to Be Alive.
Kupitia akaunti ya Instagram wa Nicki Minaj, aliweka tuzo hiyo na kuandika kwamba ‘Albamu bora ya Rap, Dreams Worth More Than Money,” aliandika mrembo huyo.
Hata hivyo, kiongozi wa Maybach Music Group, Rick Ross, alitumia akaunti yake ya Twitter kumpongeza msanii huyo ambaye yupo naye kundi moja.